Thursday, August 28, 2014

Umeisoma ripoti ya leo kuhusu chai na chakula kwenye bunge la katiba? Nishiida!!

Gazeti la Mtanzania August 28 2014 ndio limeripoti hii stori kuhusu Bunge la Katiba linaloendelea Dodoma, kikubwa ni gharama mbalimbali zinazotumiwa na Wajumbe. Wameandika bunge la katiba lateketeza mamilioni ya fedha ambapo kikombe cha chai na biskuti au karanga kinalipiwa shilingi elfu 10 kila siku kwa kila Mjumbe mmoja licha ya kwamba kila Mjumbe anapokea posho ya siku ambayo ni laki mbili na elfu 30. Kwenye sentensi ya pili wameandika, chakula cha mchana kila Mjumbe analipiwa elfu 16 kwa siku ambapo kwa siku hiyohiyo iendayo kwa Mungu, ni shilingi milioni 8 hulipwa kama gharama za ukumbi wa kufanyia mikutano

Hungana na familia ya kihabari kwa ku BONYA HAPA 


Posted via Blogaway

PICHAZ: K LYINN NI MREMBO WA KUZALIWA …TAZAMA PICHA HIZI!!

Q-Jay kusikika tena kwenye bongo fleva baada ya ukimya mrefu toka aokoke

Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye muziki huo katika wimbo mpya. Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q- Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’, ambao ni wa kuhamasisha amani. Miaka kadhaa iliyopita Q-Jay aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Sifai’, aliamua kuachana na muziki wa kidunia baada ya kuokoka na kutangaza kuwa atakuwa akifanya muziki wa gospel.

Ungana na familia ya habari kwa ku BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO ALHAMISI ZIPO HAPA

Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 50 kumtaka Edinson Cavani kutoka Paris St-Germain, kutokana na Olivier Giroud kuwa na uwezekano wa kutocheza kwa muda mrefu kutokana na jeraha la mguu (Daily Express), Arsenal pia wanamtaka Danny Welbeck, 23, kutoka Manchester United, kuziba nafasi ya Giroud, lakini Man U wanasita kumuuza Welbeck (Daily Mail), boss wa Arsenal vilevile anataka kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco, na pia Loic Remy, 27, ambaye anapatikana kwa pauni milioni 8.5 kutoka QPR (the Guardian), boss wa Manchester United Louis van Gaal anafikiria kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Joe Allen, 24, kwa kutoa pauni milioni 20, (Daily Star), United wanafanya mazungumzo ya kumsajili Daley Blind, 24, huku kipa wa zamani wa Man U, Edwin van der Sar akiwa Manchester kukamilisha uhamisho wa beki huyo wa Ajax (Daily Star), Manchester United pia wanafikiria kumtoa Shinji Kagawa, 25, au Javier Hernandez, 26, kama chambo katika mkataba wa kumchukua kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, (Independent), Real Madrid watatumia kiasi kikubwa cha fedha za mauzo ya Angel Di Maria, kumnunua mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao (Le Sport), AC Milan wamethibitisha kuwa wanataka kuwasajili Fernando Torres, 30, na kiungo Marco van Ginkel, 21 kutoka Chelsea (Daily Express), AC Milan wamechoka kumsubiri Torres kuamua anataka nini na wamempa makataa, huku wakijiandaa kuanza kumfuatilia Roberto Soldado, 29, kutoka Tottenham au Fabio Borini, 23, wa Liverpool (Inside Futbol), Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa Sevilla Federico Fazio, 27, baada ya kulipa pauni milioni 8 za kipengele cha ununuzi (Daily Telegraph), Spurs pia wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka Cameroon Alexandre Song, 26, ambaye ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona bure (the Times), boss wa QPR Harry Redknapp yuko tayari kupanda dau kwa kiungo wa West Ham Mohammed Diame, 27, (Daily Mirror), Alvaro Arbeloa anataka kuondoka Real Madrid kabla ya dirisha la usajili halijafungwa (El Chiringuito), Manchester United wanajiandaa kutoa dau jipya la pauni milioni 33.4 kwa Juventus kumtaka Arturo Vidal (Gazzetta dello Sport), Real Madrid watapambana na Barcelona na Atletico Madrid kutaka kumsajili Marco Reus kutoka Borussia Dortmund (AS), Hatem Ben Arfa anataka kubakia Newcastle licha ya meneja Alan Pardew kutompanga (Newcastle Evening Chronicle), Arsene Wenger anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Birmingham City, Nikola Zigic ambaye ni mchezaji huru (www.zurnal.rs). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Zimesalia siku tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Source salim kikeke

Posted via Blogaway

AY na Diamond wadai watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri kimuziki

AY amedai kuwa kuwa yeye na Diamond watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri baada ya kuyumba hapo awali. AY ameiambia Bongo5 kuwa kama ilivyo kawaida yake kumsaidia msanii mmoja kila mwaka, mwaka huu atahakikisha Chidi anakaa pazuri. “Huwa nina uhakika wa kufanya comeback nzuri tu, sio kwamba ninavyomsupport Chidi tunapata faida yoyote. Kila mwaka huwa ninampick mtu mmoja, so mimi na Diamond tuliamua kuwekeza kwenye audio pamoja na kufanya naye video pamoja kwa gharama zetu sisi. Kama unavyoona promotion yake, mpaka sasa hivi tupo kwenye process ya kufanya video. Bado hatujajua tutafanya wapi video ila tupo kwenye maandalizi ya mavazi, location na mambo mengine,”amesema AY. Hivi karibuni Chidi Benz alitoa wimbo ‘Mpaka Kuchee’ aliowashirikisha AY na Diamond.

Kama bado ujajiunga nasi BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

HIZI 3D TATOO LAZIMA UZITAZAME KWAMAKINI...VINGINEVYO UTADHANI UONGO!!!!