Sunday, August 10, 2014

Haya ndiyo mavazi wanayovaa wahudumu wa ndege kujikinga na Ebola

Ugonjwa wa Ebola umelipuka sana huko Africa magharibi na umeua watu wengi sana. Hivi sasa mambo mengi yanafanywa ili kukinga watu dhidi ya maambuzi mampya. Njia moja wapo ni kutenga na kulifunga eneo lolote ambalo lina mgonjwa wa Ebola. Lakini hivi ndivyo wafanyakazi wa ndege za Africa magharibi wanavyovaa ili kujikinga.

Saturday, August 09, 2014

PICHA : BAHATI BUKUKU SASA MZIMA WA AFYA NJEMA, AMTUKUZA MUNGU

''(Sina maneno ya kusema zaidi ya
kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake, pia nawashukuru watu wote walioniombea pamoja na waliokuja kuniona hata wale
ambao wameshindwa kufika, kwani najua walikuwa wakiniombea)'' Hayo ni baadhi ya maneno ya muimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku, akiieleza
GK, kutokana na ajali aliyopata usiku wa kuamkia tarehe 26 Julai 2014.

Stori mpya kuhusu daraja la Kigamboni na kivuko kipya.

Waziri wa Ujenzi John Magufuli amesema Serikali inatarajia kuongeza kivuko kingine cha kuvusha watu Kigamboni ambacho kitagharimu shilingi bilioni 3.7 wakati ujenzi wa daraja ukiendelea.

Anasema daraja linalojengwa sasa hivi litakamilika June 2015 badala ya July kama ilivyokua imefahamika mwanzoni ambapo tayari Mkandarasi ameshalipwa shilingi Bilioni 117 kati ya 214 za kukamilisha mradi wote limeandika gazeti la Tanzania Daima.

Nalo gazeti la HabariLEO August 9 2014 limeandika >> Magufuli abana wenye magari Kigamboni, ataka wasisumbue abiria wa Pantoni asubuhi na jioni, wenye haraka watakiwa kuzunguka Kongowe – Mbagala, ni agizo la muda mfupi baada ya kivuko kilichopo kuzidiwa.

 SOMA STORY NYINGINE KWA KUBONYA HAPA 


Posted via Blogaway

HIVI KWA NINI WASANII WENGI WA BONGO NI WAFUPI???? HAWA NI BAADHI YAO.

Nimefanya uchunguzi mdogo tu nimegundua kuwa wasanii wengi wa music Tanzania ni wafupi, sijui kwanini? Au kuna uhusiano wowote ule kati ya ufupi na kipaji? Au ndio ile theory ya kwamba watu wafupi wanapenda sana kujionyesha kwakuwa wanahisi wanadharaulika?

Wafuatao ni baadhi tu kati ya wale wengi:
1. Barnaba Boy
2. Stamina
3. Linnah
4. Sheta
5. Rich Mavoko
6. Nikki wa Pili
7. T.I.D
8. Ommy Dimpoz
9. Dully Sykes
10. Ally Kiba
11. Young Dee
12. Vanesa Mdee

KWANINI WASANII WENGI WA BONGO WAFUPI?

 BONYEZA HAPA KUTOA MAONI YAKO 


Posted via Blogaway

Angalia picha ya Wema na Jokate walipokutana kwenye ndege leo

Jokate aliwahi kukiri kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond kwa muda
usiozidi miezi miwili ambapo wakati yuko na Diamond zilitoka stori nyingi pia kuhusu uhusiano wa Wema na Jokate kuingia
matatizoni.

Ni stori ambazo ziliandikwa sana na inawezekana mpaka leo watu wengine walikua wanaamini Jokate na Wema hawawezi kukaa
meza moja ila Aug 9 2014 Wema Sepetubbaada ya kuwasili Mwanza kwa ajili ya show ya
Serengeti Fiesta 2014 baadae CCM Kirumba amepost hii picha.
Wakiwa kwenye ndege ya Fastjet Wema na Jokate wakitokea Dar es salaam walipiga selfie
ambayo Wema ameipost kwenye instagram page yake na kuandika hayo maneno hapo chini akimaanisha wako poa sasa hivi.

 STORY ZINGINE SOMA KWA KUBONYA HAPA 


Posted via Blogaway

BABA MZAZI AMPA UJAUZITO MWANAYE,WANANZENGO WAJA JUU

Mkazi wa Kijiji cha Bwekela wilayani Igunga mkoani Tabora, Kashinje Shima, anatafutwa na Uongozi wa kijiji hicho, kwa kumpa ujauzito mwanawe wa kumzaa mwenye umri wa miaka 17. 
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igoweko, Robert Ruhende, alilaani kitendo kilichofanywa na mzazi wa mtoto huyo na kusisitiza kuwa sheria lazima ichukue mkondo wake.

Akisimulia kisa hicho, mke wa mkazi huyo ambaye pia ndiye mama mzazi wa mtoto huyo, Geni Njiro, alidai alibaini hali hiyo Julai 23 mwaka huu, baada ya mwanawe wa kiume kumfumania baba yake na dada yake.

Kwa sasa kwa mujibu wa Geni, mwanawe huyo ambaye inadaiwa amekiri kushiriki kitendo hicho, ana ujauzito wa miezi saba.

Geni alidai kabla ya kugundua kitendo hicho cha kinyama kilichokuwa kikifanywa na mumewe, alihisi kuwa baba wa mtoto huyo alikuwa akitumia mwanya wa yeye mama kutokuwepo nyumbani, kufanya vitu visivyo vya kawaida.

Alidai kuwa alipata hofu kuhusu mwenendo wa mumewe na mtoto wake siku moja walipokuwa shambani wakiendelea na shughuli za kuvuna mazao,  ambapo mumewe aliaga kurudi nyumbani.

Kutokana na hofu hiyo, Geni alidai aliamua kumtuma mtoto wake mkubwa wa kiume, ambaye hakutaka kumtaja jina, akafuatilie nyumbani kupata uhakika wa kile alichokuwa akihofia.

Mama huyo alidai baada ya mtoto wake huyo  kufika nyumbani, ndipo alikuta baba yake wakifanya ngono na mdogo wake na kurudi shambani na kumpa taarifa mama yake.

Baada ya taarifa hiyo, mama huyo alidai kuwa aliamua kuita ndugu wa pande zote mbili, kwa ajili ya kuzungumzia unyama huo, ambapo baba huyo alipohojiwa katika kikao hicho cha  familia, alikana kuhusika na tuhuma hizo.

Hata hivyo, mama huyo alidai babu wa mtoto huyo, alishauri waende kupima hospitali kupata ukweli, ndipo baba huyo alipokubali kuwa anatembea na mtoto wake.

Baada ya kukubali, inadaiwa baba huyo alitakiwa kulipa adhabu ya faini ya ng’ombe wawili, ambao aliwalipa na suala hilo kuwa limekwisha.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwina, Bundala Makelema, alikiri kuwepo kwa suala hilo.

Alidai kuwa wakati mtuhumiwa huyo akilipa adhabu ya kimila ya ng’ombe wawili, yeye alishiriki kwa nafasi yake ya Kiongozi wa Kitongoji.

Hata hivyo, inadaiwa familia anayotoka mama huyo, ilipinga uamuzi huo wa kifamilia na kumruhusu ndugu yao, kuchukua hatua zaidi, ikiwemo kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilipofika kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igoweko, Ruhende ambaye aliahidi kwenda Polisi ili hatua zaidi zichukuliwe, mama huyo alidai ndipo mumewe alipoamua kutoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.

>>malunde1 blog

 STORY ZINGINE ZIPO HAPA bonya hapa 


Posted via Blogaway

KIBONDE WA CLOUDS KAMA HIKI ULICHOKIFANYA NI KWELI, BASI UMEJITIA AIBU. KUWAKIMBIA TRAFKI

Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma.

Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge.

Trafiki aliingia ktk gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke ktk gari lake, trafiki naye kagoma kushuka.

Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo.

Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo.

Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema ananigonga, afande, ananigonga! Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi kanisani, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa 'TINGASI'!


Posted via Blogaway

HATA KAMA NI MAPENZI HAYA YAMEZIDI SASA, DIAMOND NA WEMA SEPETU WAPIGANA DENDA HADHARANI BILA HATA AIBU, TAZAMA PICHA HAPA

Mara baada ya kutua Mwanza hii ndiyo picha ya kwanza aliyopost Martin Kadinda ikimuonesha Diamond Na Wema Sepetu
wakipigana Denda mbele za watu bila hata
aibu..!!

 BONYEZA HAPA KUSOMA STORY MBALIMBALI 


Posted via Blogaway

HABARI MBAYA KWA WAPENZI WA ORIJINO KOMEDI, YADAIWA KUNDI HILO LIMEVUNJIKA.

Hakuna ubishi kua miaka michache iliyopita kund la Orijino Komedi ndio lenye mashabiki wengi hapa nchini. Ilikua ikifika mda wa kurushwa kipindi kila mtu alikua hangoki katika TV yake. Umaarufu wao uliongezeka zaid pale walipohama EATV na kuhamia TBC.

Umaarufu wao uliendelea kuwepo hadi siku za karibuni ambapo ulishuka kwa kasi sana, taarifa ambazo Bongoclan tumezipata ni kua kwa sasa kundi hilo limevunjika na kila mtu anafanya kazi kivyake.

Chanzo chetu kutoka kituo cha TV walichokua wakifanya kazi kiasema kua kwa sasa kila mtu ana hamsini zake na hawafanyi kazi tena pamoja.

 SOMA STORY NYINGINE KWA KUBONYA HAPA 


Posted via Blogaway

Picha 5 za ajali ya kuungua kwa basi la 5 Aliance leo August 09.

Hili ni basi la kampuni ya 5 Aliance ambalo linafanya safari zake kati ya Mtwara na Dar es salaam limeungua asubuhi ya August 09 likitokea Mtwara kuelekea Dar es salaam.

Taarifa ya awali inasema kuwa hakuna abiria aliyepata madhara yoyote juu ya kuungua kwa basi hili ambalo limeteketea kijiji cha Mihambwe mkoa wa Lindi.