Saturday, August 09, 2014

ANGALIA PICHA NATURE ALIVOPIGA SHOO YA NGUVU TAIFA

Nature na kundi lake la Wanaume Halisi wakifanya vitu vyao .
Mwanamuziki Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi wakifanya yao ndani ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 Uwanja wa Taifa.
Nature akiwadatisha mashabiki wake.

Source gp

MADEE AMTAFUTA ALIYEMWAGA POMBE YAKE NDANI YA TAMASHA LA MATUMAINI 2014

Madee akisema na mashabiki wake.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Kundi la Tip Top Connection, Ahmad Ally ' Madee' akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 .
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Madee.

Source gp

WATU NA MASHEPU YAO,, UKO INSTERGRAM... TAZAMA PICHA UTAKUBALI TU

Meninah
Vera sidika

BARCELONA YAIPIKU MANCHESTER UNITED USAJILI WA THOMAS VERMAELEN

Wamekubaliana: Barcelona wameonekana kuwapiku Manchester United katika kumsajili, Thomas Vermaelen. BARCELONA imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 ili kuinasa saini ya beki wa Asernal, Thomas Vermaelen, na taarifa hizi ni pigo kubwa kwa mashetani wekundu, Manchester United waliotaka kumsajili.

Kilichobaki sasa ni makubaliani binafsi kati ya wakala wa Vermaelen na wakatalunya hao kabla ya kukamilika kwa dili hilo.

Jana jumatano, Barcelona walimtuma Raul Sanllehi kufanya makubaliano mjini London na wamefikia sehemu nzuri.

Wakatalunya wametoa ofa ya miaka mitano, huku kukiwepo kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi na mshahara wa beki huyo utakuwa paundi elfu themanini.

Mazingira mapya? Barcelona wanaonekana kuelekea kumsajili Vermaelen kwa mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi elfu 80.

Hakuna kwenda: Arsenal walitaka kumuuza Vermaelen Man United kwa kubadilishana na Chris Smalling.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA 

YANGA ( WABUNGE) WALIVYOISAMBARATISHA SIMBA ( WABUNGE) KATIKA TAMASHA LA MATUMAINI 2014

Mashabiki wakifuatilia mtanange huo .
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba
Mwigulu Nchemba akiwarushia skafu yake mashabiki wa Yanga .
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni shabiki wa Yanga , Ridhiwan Kikwete akivua jezi yake kwa ajili ya mashabiki mara baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3 - 2 dhidi ya Simba leo .
Naibu Waziri wa Fedha , Mwigulu Nchemba akishangilia na shabiki wake baada ya ushindi wa Yanga

Source globalpublisher

Friday, August 08, 2014

‘ SIMBA SC DAY ’ HAWA NDIYO WACHEZAJI WALIOSAJILIWA KUELEKEA MSIMU MPYA 2014/15

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,

Hussein Shariff, Manyika Peter Manyika, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Elius Maguli, Saad Kipanga watatambulishwa kesho katika Tamasha la ‘ Simba Day’ katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tamasha hilo la kila mwaka ambalo hufanyika tarehe 8, Agosti ya kila mwaka lilianza kufanyika kwa mara kwanza msimu wa kiangazi mwaka 2009 chini ya waasisi, Mzee Hassani Dalali na aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwa lengo la kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya za klabu huku pia lengo kiuchumi likiwemo .

Wachezaji hao wazawa wataungana na wachezaji wapya wa kigeni, Paul Kiongera raia wa Kenya, Mrundi, Pierre Kwizera, na washambuliaj raia wa Botswana, Jerome Ramathakwane na Ousainou Manneh kutoka nchini Gambia katika mchezo maalumu dhidi ya Zesco ya Zambia.

Ambao watajaribiwa kwanza na kocha Zdravko Logarusic kabla ya kusajiliwa. Hussein Sharrif Tamasha hilo litafanyika kesho Agosti 9, kufuatia siku ya leo kuwa na Tamasha la Matumaini na mashabiki wa Simba watapata fursa ya kuona na kununua jezi mpya za klabu hiyo ambazo watazitumia msimu ujao.

Simba imejipanga kuhakikisha inaimarisha zaidi kikosi chake ndiyo maana wamekuwa ‘ busy’ kusaka wachezaji wakati huu dirisha la usajili likikaribia kufungwa.

WACHEZAJI SABA WA KIGENI Donald Musoti, Amis Tambwe, Joseph Owino, Kiongera, Kwizera, Jerome, na Manneh watakuwepo uwanjani siku ya kesho.

Wachezaji hao wote ni raia wa kigeni na wamekuja kwa ajili ya kuifufua Simba baada ya kuwa na misimu miwili mibaya katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Simba inaweza kuwasaini wachezaji wote hao kama mwalimu Logarusic ataridhika na viwango vyao kwa sababu sheria ya wachezaji wa kulipwa itabadilishwa na kufikia wachezaji saba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tamasha la Simba Day kuwa na wachezaji saba wa kigeni na ni wakati mwafaka kwa mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza uwanjani siku ya kesho kwa lengo la kwenda kuitazama timu yao mpya ambayo inasukwa katika mtindo wa kimataifa.

Ligi kuu inataraji kuanza kutimua vumbi lake, Septemba 20, hivyo baada ya Tamasha hilo timu itakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na kutengeneza timu kabambe ambayo itaweza kutoa ushindani kwa timu za Yanga SC, Azam SC, Mbeya City ambazo zimeoneka kufanya usajili makini zaidi licha ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimu uliopita.

Wachezaji kama nahodha Nasorro Masoud ‘ Collo’, Amri Kiemba, Issa Rashid, William Lucian, Jonas Mkude, Said Ndemla, Miraji Adam, Abdallah Seseme, Ibrahimu Twaha, Ramadhani Singano, Haroun Chanongo, Uhuru Suleimani, Ivo Mapunda wataungana na wachezaji wapya waliosajiliwa klabuni hapo siku ya kesho huku mwanamuziki nyota nchini, Diamond Platnumz akitaraji kutumbuiza kabla ya zoezi la utambulisho wa wachezaji kuanza.

Itakuwa siku ya aina yake kwa wapenzi wa klabu hiyo. NI SIKU NZURI KWA KUSAIDIA UJENZI WA UWANJA WA KLABU Wiki iliyopita Simba ilianza kufanya mazoezi katika uwanja wake wa wazi huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na juzi wanachama wa tawi la ‘ Home Boys Wazo Hill’ waliahidi kutoa tani 10 za mifuko ya saruji ili kusaidia uendelezaji wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo ambao unaendelea.

Simba inaweza kutumia Tamasha hilo kuwaunganisha wanachama wake ambao walikuwa katika tofauti miaka ya karibuni kutokana na uongozi mbaya wa utawala uliopita. Kila mwanachama wa Simba anaweza kujitolea kwa namna anavyoweza kwa sababu wanachama ndiyo sehemu muhimu ya kuijenga klabu hivyo ushirikiano ni muhimu kuanzia kwa viongozi, wanachama, wachezaji na benchi la ufundi.

Simba Day ina maana kubwa na wanachama wanaweza kutumia nafasi yao kusaidia kwa hali na mali klabu yao. Kila la heri Tamasha la Simba Day….. 0714 08 43 08

HIKI NDICHO KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHACHOJITUPA LEO UWANJANI KUMENYANA NA RAYON SPORT

Timu ya Azam FC leo tarehe 08. 08. 2014 inajitupa kiwanjani hapa mjini Kigali Rwanda katika mchezo wake wa Kwanza dhidi ya Rayon Sport, katika mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENG CUP.
Wanaotuwakilisha leo ni hawa hapa
1. MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. GADIEL MICHAEL
4. DAVID MWANTIKA
5. AGGREY MORISii
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. JOHN BOCCO
10 KIPRE TCHETCHE
11. KHAMISI MCHA
AKIBA
AISHI MANULA
MUDATHIR YAHYA
SAID MORAD
ABDALLAH KHERI
FARID MUSSA
DIDIER KAVUMBAGU

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Azam FC.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA  

RIDHIWANI KIKWETE AAPISHWA KUWA WAKILI

Mke wa Rais Mama salma Kikwete, akimpongeza mwanae, Ridhiwani Kikwete, kwa kumpa shada la maua baada ya kutunukiwa Cheti cha kuwa Wakili wa kujitegemea, wakati wa hafla ya kuwatunuku mawakili 128, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akamata #10 katika orodha ya viongozi wanaofanya vizuri Afrika, Rais wa Mali aongoza

Rais Jakaya Kikwete, amekamata nafasi ya 10 katika orodha ya viongozi wa nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la Sahara kwa mujibu wa survey iliyofanywa na kampuni ya maoni ya Gallup.

Nafasi ya kwanza imekamatwa na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita na kufuatiwa na Ian Kahama wa Botswana. Nafasi ya tatu imekamatwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akifuatiwa na Rais wa Cameroon, Paul Biya. Naye Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 27 amekamata nafasi ya 9.

Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani kwa 26 amekamata nafasi ya 21 wakati Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo akikamata nafasi ya 24.

 BONYEZA HAPA KAMA BADO UJAJIUNGA NASI 

AMANDA POSHY AMEVUTIWA NA ALI KIBA SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Mcheza filamu mwenye umbo amabalo linawachanganya wanaume wengi wa kwale Amanda Poshy ameshindwa kujizui hisia zake na kujikuta akitupia ujumbe wenye maneno ya wimbo wa Ali kiba kwenye akaunti yake ya facebook ameandika

"Amesema sana mama,dunia tambara bovu...kuna asali na shubiri..ujana ,giza na nuru...(Maneno ya kiba hayo)yana maana kubwa sana ukiisikiliza nyimbo nzima ila me pamenivutia hapo tu"

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA  

ABDI BANDA AWAINGIZA SIMBA SC ‘CHOO CHA KIKE’

Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi akiwaonesha wanahabari baadhi ya vifungu vya mkataba wa Banda wakati wa mkutano na wanahabari jana klabuni Coastal Union .

Na Mwandishi Wetu, Tanga UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umekiri kupokea barua kutoka kitengo cha Wanasheria (Maleta & Ndumbaro Advocate cha Dar) ikisema kuwa timu hiyo imeshindwa kumlipa Abdi Banda mshahara wa miezi mitatu mfululizo na kusema imevunja mkataba.

Akizungumza jana,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amekanusha na kuwa habari zilizoenezwa kwamba walishindwa kumlipa mshahara mchezaji huyo sio za kweli bali kilichotokea ni kwamba Banda alifundishwa na watu wajinga asichukue mishahara yake ya miezi mitatu ili kukipa hadhi kipengele hicho cha sheria kilichopo kwenye mkataba wake, “Akinukuu kipengele cha ibara ya 3(3.2)(1) cha mkataba wa Banda kinachosema kuwa ikiwa klabu imeshindwa kumlipa mchezaji mishahara yake ya miezi mitatu mfululizo basi mkataba wa mchezaji huyo na klabu umevunjika “Alisema El Siagi.

Alisema alichokifanya mchezaji Banda ni kukwepa kuchukua mishahara yake makusudi ili ionekane kwamba hakulipwa miezi mitatu . El Siagi alisema alichokifanya ni mambo mawili, jambo la kwanza ni kudanganya wanamichezo hapa nchini na klabu yake ya Coastal Union ili aipatie fedha Klabu ya Simba ambapo huo ni Wizi wa kutumia hila.

Alisema la pili ni kitendo cha kusaini mkataba Simba wakati akijua ana mkataba na Coastal Union ambao unatarajiwa kuishia Juni 2016. Katibu huyo alisema ni makosa makubwa mchezaji huyo kusaini mikataba miwili tofauti katika kipindi cha msimu mmoja kwa sababu atakuwa amevunja taratibu za mikataba kutokana na kuwa mchezaji hawezi kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja.

Aidha alisema kutokana na mchezaji huyo kudanganya na kukiuka utaratibu wa mkataba, Uongozi wa Coastal Union umejipanga kumchukulia hatua kali mchezaji huyo ikiwemo hatua za kinidhamu.

Katibu huyo alisema anashangazwa kuona kuwa klabu ya Simba yenye viongozi wazoefu kwenye masuala ya mpira wanafanya makosa kama hayo kwa kutokufuata taratibu za kiusajili.

“Kanuni za shirikisho la soka Dunia (FIFA) na Shirikisho la soka nchini (TFF) zinasema mchezaji hawezi kuzungumza na timu yoyote wakati akiwa ndani ya mkataba mpaka labda awe amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake ndio anaruhusiwa kuzungumza na uongozi wa klabu nyingine.

Aliongeza kuwa iwapo mchezaji akiwa amebakiza mwaka mmoja basi klabu na klabu ndio zinaruhusiwa kuongea na sio mchezaji hivyo Banda bado ana miaka miwili Coastal Union ambayo imebaki hivyo Simba walichotakiwa kufanya ni kuzungumza na uongozi wa Coastal union ili kumnunua mkataba wake badala ya kurubuniwa na kauli hafifu za kiudanyanyifu.

Katibu huyo alisema kwa kufanya hivyo Coastal Union kupitia wanasheria wake ,Divine Chambers Advocates & Hamidu Mbwezeleni wanajipanga kuwaandikia barua shirikisho la soka nchini (TFF) pamoja na Simba ili kudai fidia ya ukiukaji wa taratibu hizo.

Alieleza kuwa tayari Coastal Union wamemtumia mwanasheria wa Banda majibu ya barua yake kupitia mwanasheria Divine Chambers Advocates ya Mjini Tanga.

Kama bado ujaungana nasi BONYEZA HAPA 

BAADA YA KUTUA BONGO..MASOGANGE ATUPIA PICHA ZA HATARI AKIUBINUA MZIGO WAKE KITANDANI ..ZIONE HAPA!!

BASI UNAAMBIWA HIZI NDO NYIMBO 10 KALI ZAID NA ZENYE UJUMBE ZILIZOWAHI KUHIT TANGU BONGOFLAVA IANZE

Muziki wa bongofleva umefanya mapinduzi sana kuanzia mwanzoni mwa miaka 2000 mpaka sasa, zifuatazo ndizo nyimbo bora za bongofleva zenye ujumbe ambazo hupaswi kuacha kuzisikiliza...

1. Dunia Njia,
hii nyimbo iliimbwa na Bushoke ni moja ya nyimbo zenye ujumbe mzito kabisa , ukiiskiliza anaelezea maisha kwa ujumla, maisha baada ya kifo na matabaka yaliyomo katika jamii,..hupaswi kuacha kuisikiliza hii nyimbo itakufunza mambo mengi

2 Kazi Yake Mola,
hii nyimbo imeimbwa na madee akishirikiana na mandojo na domokaya, kazi yake mola ni nyimbo inayohuzinisha kwa upande mmoja ila inafunza mambo mengi mnoo

3 Siku Hazigandi,
Malkia wa muziki wa bongofleva Jide akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao murua kabisa, achilia mbali midundo inayopatikana humu, ujumbe unaopatikana ni mkubwa sana unalenga kumfanya msikilizaji ajifunze kutokata tamaa katika maisha....

4 Ndio Mzee,
Professor J akiwa katika ubora wake alitunga hichi kibao ambacho kinakuelezea mustakabali mzima wa siasa na demokrasia ya kiafrika kwa kutumia lugha ya kiswahili, hii nyimbo inakufanya upate utashi mkubwa sana wa siasa za kiafrika na Tanzania....namshukuru Mungu nimebahatika kuisikia hii nyimbo

5 Darubini Kali,
Afande sele akishirikiana na Dogo ditto walitoa hichi kibao kilichomfanya Afande sele kuwa mfalme wa rhymes, kaongelea mambo mengi sana humu , ni moja ya nyimbo bora kabisa kuwahi kutungwa nchini Tanzania

6 Alikufa kwa Ngoma
Mwanafalsafa akishirikiana na Jide walitoa hichi kibao katika kipindi ambacho gonjwa la ukimwi lilikuwa tishio mno, aina ya ujumbe na uwasilishwaji wake kunaifanya hii nyimbo kuwa ya tofauti miongoni mwa nyimbo zote zilizokuwa zinaongelea kuhusu ukimwi,,,, hupaswi kuacha kutoiskiliza hii nyimbo

7 Mapenzi Kitu Gani,

huwezi ukazungumzia maisha ya mwandamu bila kuhusisha na mapenzi, MB DOGG akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao kujaribu kuonyesha uwalakini wa neno mapenzi, uhusiano wa utajiri, umaskini, umaarufu na mapenzi...ujumbe japo ni wa mapenzi lakini ni mzito mno....ni moja ya nyimbo bora kabisa za mapenzi hapa Tanzania

8 Elimu Dunia,

Daz baba aliachia kibao hichi ambacho ndani yake ujumbe wake unalenga kufundisha umuhimu wa elimu, hii nyimbo ni nzuri mno hupaswi kuacha kuisikiliza..

9 Sihitaji marafiki,

Farid kubanda nyimbo zake zote zina ujumbe mkali, ila ujumbe unaopatikana katika hii nyimbo ni wa kitofauti na wa kipekee,, kama nyimbo inavyojieleza "sihitaji marafiki'.......

10 Hii ndiyo Tanzania

Unataka kufahamu mambo ya Tanzania basi nenda kaisikilize hii nyimbo ya Roma mkatoliki inayoitwa "hii ndiyo Tanzania".........utapata ujumbe mzit sana aseee

Nadhani hizi ndizo nyimbo muhimu zaidi kwa Mtanzania yeyote kuisikiliza ....kama kuna ambayo imesahaulika au unalist yako hebu itaje hapa tuijadili. BONYEZA HAPA 

DUNIA INAKWENDA WAP?!!VTAZAMA DOCUMENTARY YA MASHOGA WAJAMAIKA WANAOJIITA GULLY QUEENS [PHOTOS]

Siku tatu zilizo pita kituo cha Television cha VICE News documentary wamerusha documnaty ya kikundi cha vijana waishio mji wa Kingston .Jamaica. Nnchini Jamaica, kuvamiwa, kubabwa,kuuwawa ni vitu vya kawaida kwa MASHOGA...Kutokana na hali hiyo wanaisha mashashaka na wapo chimbo wamejificha ....hebu cheki baadhi ya picha za LAIFU STAILI yao...

JISOMEE MWENYEWE JINSI SHILOLE ALIVOSHAMBULIWA INSTA BAADA YA KUPOSTI PICHA HII

Shilole Alipost Picha hiyo hapo juuu na Kuandika Maneno haya "Baada ya Kutoka TBC tv Taifa! Now nipo Mlimani Tv Live "
Jisomee Watu walivyomchamba hapa chini:

Kauli ya CHADEMA kuhusu taarifa za Wabunge wake 'kuonekana Dodoma'

Kumekuwepo na madai yanayosambazwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari kuhusu baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuonekana mjini Dodoma au kujisajili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini humo.
Chama kupitia Idara ya Habari kingependa kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;

1. Uamuzi wa kuwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaotokana na CHADEMA kushirikiana na wenzao wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kutoshiriki vikao vya bunge hilo ili kuepuka kunajisi mchakato wa Katiba Mpya, ulitokana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu iliyoketi Julai 18-19 na kuazimia kwamba;
Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na CHADEMA, kama sehemu ya UKAWA, watarudi kwenye vikao vya Bunge Maalum endapo tu mamlaka ya Bunge hilo yatafafanuliwa kuwa ni ya kuboresha, na sio kuibomoa au kuifuta, misingi mikuu (basic features) ya Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi na kuandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoteuliwa na Rais kwa ajili hiyo;
Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na CHADEMA, kama sehemu ya UKAWA, watarudi kwenye vikao vya Bunge Maalum endapo tu, na baada ya, ufafanuzi uliotajwa katika aya ya 2 utahusisha marekebisho ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, inayohusu mamlaka ya Bunge Maalum, pamoja na Kanuni husika za Bunge Maalum;
Wajumbe wote wa CHADEMA katika Bunge Maalum hawatashiriki katika kikao chochote cha Bunge Maalum au Kamati zake hadi hapo ufafanuzi wa mamlaka ya Bunge Maalum uliotajwa katika aya za 2 na 3 utakapofanyika kwa mujibu wa maazimjo ya Kamati Kuu;
Hadi wakati huu, hakuna jambo hata moja kati ya hayo lililofanyika, huku mazungumzo yaliyotarajiwa kuokoa mchakato yakiwa yamevunjika, kwa sababu CCM na Serikali yake wameamua kudharau na kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba badala yake kuweka maslahi ya chama hicho kwenye katiba.

2. Iwapo kuna mjumbe/wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaotokana na CHADEMA wameonekana wakijisajili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma au watashiriki vikao vya bunge hilo au kamati zake, wataandikiwa barua ya kujieleza kisha chama kitachukua hatua kwa mujibu wa taratibu zake kupitia vikao.

3. Tunapenda pia kuwakumbusha wanachama wa CHADEMA na umma mkubwa wa Watanzania kuwa, mji wa Dodoma mbali ya kuwa Makao Makuu ya Nchi pia inapatikana Ofisi Kuu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba ambako hakujaridhiwa na Watanzania wengi, hakujazuia shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanyika ikiwemo kutoa huduma kwa watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wabunge. Suala hilo linakwenda sambamba na ukweli kwamba sehemu kubwa ya watumishi wa Bunge Maalum la Katiba ni wale wale ambao wanatakiwa kuwahudumia wabunge wa Bunge Maalum la Katiba.

Hivyo kuonekana kwa mbunge yeyote wa CHADEMA mjini Dodoma au kwenye viwanja au Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuwezi kutafsiriwa moja kwa moja kuwa mbunge husika amehudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba, kinyume na msimamo wa UKAWA.

Imetolewa leo Alhamis Agosti 7, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari - CHADEMA

 BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA PAGE YETU 

Dogo Janja apiga chini masomo ya sekondari, aamua kusomea muziki

Rapper wa Arusha aliyerejea tena Tip Top Connection, Dogo Janja amedai kuwa haoni umuhimu wa kuendelea na masomo ya sekondari na hivyo ameamua kusomea muziki.

Akizungumza na Bongo5 jana akiwa jijini Mwanza kwaajili ya Serengeti Fiesta 2014, Dogo Janja amedai kuwa tayari ameshaanza mafunzo ya kutumia vyombo vya muziki kama vinanda. “Mimi napenda sana muziki, shule yenyewe basi nitaangalia mbeleni huko,” amesema rapper huyo.

“Mimi hakuna maishani kwangu ninachokipenda kama muziki,nataka kwenda kusomea muziki, nishaanza kupiga vinanda, kuna chuo cha muziki na kuna mwalimu ananifunza anaitwa David.

Kwahiyo nitaongeza juhudi zaidi kwenye kujifunza muziki kwa sababu ni kitu ambacho nakiweza na ninakipenda. Wadau wangu na wapenzi wa burudani wasubiri ujio wangu mpya ambao utakuwa   na muziki mzuri,” ameongeza.

Source bongo 5

 BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI ILI HUPATE HABARI KIRAHISI ZAID 

PEPE REINA ATUA BAYERN MUNICH, KUSAINI MKATABA LEO

Mambo dole: Pepe Reina amekamilisha vipimo vya afya Bayern Munic. PEPE Reina anasaini mkataba wa kuitumia klabu ya Bayern Munich leo ijumaa baada ya kufuzu vipimo vya Afya klabuni hapo.

Mlinda mlango huyo amefuzu vipimo vya afya katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo baada ya Liverpool kukubali kumuuza Mhispania huyo kwa paundi milioni 20.

Reina amekosa mvuto katika miaka ya karibuni Anfield na msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Napoli. Bayern Munich walitweet jana usiku kuwa: Karibu Munich @PReina25! vipimo vya afya vimefanikiwa, mkataba utasainiwa kesho (leo).

Reina alikuwa kipa namba moja wa Liverpool baada ya kuwasili kutokea Villarreal mwaka 2006, na kucheza fainali ya UEFA. Lakini baada ya Brendan Rodgers kumleta kipa wa Sunderland msimu uliopita, nafasi yake ilipotea.

Reina ameonesha kiwango cha juu akicheza kwa mkopo Napoli na sasa anakwenda kushindana na kipa namba moja wa Bayern Neuer

 BONYEZA HAPA KUSOMA SIMULIZI MBALIMBALI ZA KUSISIMUA 

RYAN GIGGS AIFUNGIA BAO MANCHESTER UNITED IKIFUMULIWA 5-1 NA SALFORD CITY

Mtaalamu: Ryan Giggs alifunga bao pekee la kufutia machozi katika kichapo cha mabao 5-1. MAGWIJI wa Manchester United wale wa kikosi cha mwaka 1992 ‘Class of 92’ walishindiliwa kipigo kizito cha mabao 5-1 dhidi ya timu ya daraja la chini ya Salford City jana usiku.

Salford ni timu ambayo inamilikiwa na magwiji, Paul Scholes, Nicky Butty na Gary na Phil Neville. Mchezo huo ulikuwa wa hisani na ulitazamwa na mashabiki wapatao 12,00 katika dimba la Aj Bell Mjini Eccles.

Katika mchezo huo, Mkongwe Ryan Giggs ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Manchester United alimtamanisha kocha wake mkuu Louis Van Gaal kwa kufunga bao moja la kufutia machozi katika kipigo hicho cha mbwa mwizi.

Pamoja na kuzidiwa kasi na vijana wa timu hiyo kutokana na umri kuwa mkubwa, lakini nyota hao wa zamani wa Man United walionesha kiwango kizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauzeeki.

Rio Ferdinand aliyesafiri kuwafundisha magwiji hao kama kocha msaidizi, alishindwa kuwanusuru na kichapo.

 BONYEZA HAPA KUSOMA SIMULIZI MBALIMBALI ZA KUSISIMUA