Saturday, August 16, 2014

HUU NI USHAURI WA BURE KUTOKA KWA H-BABA KWENDA KWA DIAMOND NA WEMA

Msanii wa muziki na filamu H.Baba ambaye yupo ndani ya ndoa na msanii mwenzake Flora Mvungi ametoa maoni yake kwa kile kinachooendelea kati ya pande mbili za kishabiki za Diamond na mpenzi wake Wema.

Kupitia ukurasa Instagram, H.Baba amesema: Tanzaniteone uyo anawaambia sina chakusema kuhusu baba yangu na mama yangu ila baba analolakuwaambia Wema na Naseeb.

Wema kapewa lawama nyingi ila asilaumiwe kwasababu kuu nyingi tu anaeweza kumuongoza Wema ni Naseeb au mama Wema na Martin, upande mwingine Wema na Daimond wanamakosa kwani wanasubiri nini kuowana kama Kweli wanapendana wangefunga ndoa yaya yote yasingetokea kusaidiana kazini ipo ata mie huwanapanda na Mama Tanzaniteone kwenye show zangu pia filamu ya wife nashiriki. ushauri wangu Diamond unaweza kumuongoza Wema vyema tuu kama mimi ninavyomuongoza Mama Tanzaniteone ninaimani unaweza kumuongoza vyema zaidi yetu sisi.

Wawili wakipendana kuingilia penzi ni inshu ila wanapendezana sana chamsingi wangesaidiana kwenye kazi zaidi kama wema anavyoonekana akitoa #saport kubwa kwa #NASEEB na naseeb aonyeshe ushirikiano kwenye mov za wema awepo pia watauza sana kama tunavyouza filamu zetu Mie namamatanzaniteone Ikitoka leo inaisha fasta.

Pia amuongoze kwenye kipindi cha WEMA SHOW mnasaidiana kwelii ata maadui wataogopa #diamond anaweza kumpandisha wema na wema anaweza kumpandisha #daimond wote mnanguvu sana mnamashabiki sana #owaneni mtulie tuuu kwani nn mnakosa mbona sisi tupo tunaishi vyema kwa uwezo wa mungu kazi tunapata mtoto tunamlea vyema hatujalala Njaa kwasababu mwanaume kazini mwanamke kazini #NDOA raha sana asikudanganye mtu unaheshimika popote palee kama #Mume wa mtu na #mke wa mtu #Muda ndo huu umriii uwoo unakwenda fanyeni yenu fasta #leo juu kesho chini #tunawapenda sana tunawatakia maisha mema yenye Furaha kama sisi apa tunafuraha Muda wote? Karibuni kwenye ndoa muone rahaaa..

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

Ndege ya India iliyokuwa na abiria 280 yashuka futi 5000 angani baada ya rubani kusinzia

Mamlaka ya anga nchini India inachunguza tukio la hatari lililotokea Agosti 8, baada ya ndege ya Jet Airways Boeing 777-300 iliposhuka angani kwa zaidi ya futi 5000 (mita 1500) kutoka kwenye urefu waliopangiwa kuruka baada ya rubani wake kusinzia.

Tukio hilo lilitokea wakati ndege hiyo ikifanya safari kutoka Mumbai, India kwenda Brussels, Ubelgiji. Times of India imeripoti kuwa rubani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo alipumzika kidogo, mapumziko ambayo kwa viwango vya kimataifa huitwa ‘controlled rest’ kwa zile ndege za masafa marefu.

Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Brussels ni masaa 9. Rubani msaidizi alitakiwa kuchukua majukumu yote ya kuongoza ndege kwa wakati huo, lakini inadaiwa rubani huyo wa kike alisema naye alikuwa busy na tablet ya ndege hivyo hakugundua ndege ilipoanza kushuka kutoka kwenye urefu wa futi 34,000 iliyotakiwa kuruka wakati wanapita Uturuki.

Kwa bahati nzuri waongozaji wa anga wa Uturuki waligundua kuwa ndege hiyo iliyokuwa katika anga lao imeshuka kwenye urefu (altitude) ambao umepangwa kwaajili ya ndege nyingine, na kumtaarifu rubani msaidizi arudi kwenye urefu waliopangiwa.

Marubani wote wawili wa ndege hiyo wamesimamishwa kupisha uchunguzi .

 BONYEZA HAPA KUJIUNGANISHA NA BLOG HII 

LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO, MAN UNITED YA VAN GAAL, CHELSEA YA MOURINHO YENYE DIEGO COSTA, LIVERPOOL BILA SUAREZ, ARSENAL MPYA NA MABINGWA MAN CITY…PATAMU HAPOO!

Kazi inaanza; Kocha Louis Van Gaal tayari kuanzisha zama mpya Manchester United leo
Mabingwa; Manchester City wanaanza kutetea taji lao
Arsenal inaingia kwenye kampeni mpya na kikosi kilichoboreshwa
Kocha Jose Mourinho anaanza kujaribu tena kuipa ubingwa wa Chelsea

LIGI KUU ya England inaanza leo na Louis van Gaal anaanzisha rasmi zama mpya Manchester United atakapoiongoza dhidi ya Swansea City Uwanja wa Old Traffford.

Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda mechi tano na sare moja katika mech za kujiandaa na msimu na sasa watu wanataka kuangalia mafanikio yake katika ligi.

Swansea ni moja kati ya timu nane ambazo msimu uliopita zilishinda mechi Old Trafford Mashetani Wekundu wakiwa chini ya kocha David Moyes aliyetupiwa virago kwa matokeo mabaya mwishoni mwa msimu. Ikumbukwe, United pia ilikutana na Swansea katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huo 2013-2014 wakiwa mabingwa watetezi na kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Liberty, siku za mwanzoni za Moyes kazini.

Matokeo hayo hayakuwa na maana, kwani mwishoni mwa msimu United ilimaliza katika nafasi ya saba.

Wayne Rooney ataiongoza United kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Nahodha Jumanne timu hiyo ikishinda mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Valencia.

United itamkosa beki wake kinda wa kushoto mwenye umri wa miaka 19 iliyemnunua kwa Pauni Milioni 27, Luke Shaw, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama.

Baada ya kuimarisha kikosi kwa kusajili nyota kadhaa wapya, kocha Arsene Wenger ataiongoza Arsenal katika mchezo wa ugenini dhidi ya Crystal Palace. Ikiwa imetoka kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji kwa kushinda Kombe la FA msimu uliopita, Arsenal ilifungua msimu vizuri kwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifumua Manchester City 3-0 wiki iliyopita.

Mchezaji mpya, Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30 kutoka Barcelona, anatarajiwa kuwamo kwenye kikosi cha leo katika mchezo wa kwanza wa ushindani sambamba na Nahodha mpya, Mikel Arteta.

Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana na wamiliki juu ya sera ya usajili.

Mabingwa wa Championship, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha Hull City Uwanja wa Loftus Road.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho. Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.

Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool, ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa mabao Luis Suarez kwa Barcelona.

Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu huu Jumatatu. Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester City na keshokutwa Burnley v Chelsea.

Na mdadisiblog/festo saimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

SHILOLE AFUNGUKA SABABU ZA KURUDIANA NA SERENGETI BOY WAKE

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema sababu kubwa ya yeye kurudiana na mpenzi wake waliyegombana, Nuhu Mziwanda ni kuombwa msamaha

Shilole alisema mpenzi wake huyo aligundua kwamba aliteswa na wivu na kusababisha wagombane hivyo alipotambua kosa lake, aliomba msamaha wakarudiana na mambo yakawa swari.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ “Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema Shilole.

Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake.

 KAMA BADO UJAUNGANA NASI BONYEZA HAPA 

Lady Jaydee ajibu tetesi za kuachana na Gadner kwa staili hii

Wanasema picha huongea maneno 1,000. Baada ya kuendelea kwa uvumi kuwa ndoa ya Lady Jaydee na Gadner G Habash imevunjika, muimbaji huyo amepost picha akionesha pete ya ndoa kwenye kidole chake.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook wa Lady Jaydee ameandika ujumba tofauti na picha lakini mashabiki wake wameelewa kuwa ni ujumbe anaoutoa kufuatia tetesi hizo.

“Kucha zimekosa rangi ya OriFlame tu, ili zing’ae zaidi ya hapo,” ameandika Lady Jaydee.

Huu ni baadhi ya ujumbe kutoka kwa mashabiki wake.

Anna Julius

Tetea ndoa yako dada, achana na maneno ya wa2.

Saumu Kinqo

eee tumeona pete bado ipo kutofautiana kwenye ndoa ni jambo lakawaida mnayamaliza na maisha yanaendelea big up

John Sosteni

Assey Inamaana ndoa iko powa jide komaa wewe mkubwa bwana kunamambo mengi sana mnatufundisha

Calvin Mpoto

Jibu la magazeti ya bongo! Hongera J hayo ni mapito tu,kelele za chura hasishindi tembo kunywa maji!

Devotha Kyaruzi

Anamaanisha ndoa yake ipo acheni udaku.she is mrs gadner jamani oneni pete yake ya ndoa.

Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

LOGA AWAZIDI UJANJA SIMBA AJIPATIA MILIONI 27 NDANI YA WIKI TATU

ALIYEKUWA Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, amewazidi ujanja Simba baada ya kufanikiwa kujipatia sh. milioni 27 kwa muda wiki tatu.

Kocha huyo alianza kuinoa Simba mwishoni mwa mwaka jana alitokea timu ya Gor Mahia ya Kenya, kwa mkataba wa miezi sita, ambayo ilimalizika baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika. Hivi karibuni uongozi wa Simba uliamua kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja na kocha huyo, ambao ulidumu kwa wiki mbili kabla ya kusitishwa kwa ajira yake.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, zilieleza kuwa kocha huyo aliutaka uongozi uliopo madarakani kumpa Dola za Marekani 16,000, sawa na mshahara wa miezi minne. Mtoa habari huyo alisema, kocha huyo alikuwa analipwa dola za Marekani 5,000 sawa na Sh. milioni 8, 492 kwa mwezi, lakini kabla ya kusaini mkataba mpya aliwataka viongozi kumpa dola elfu 16 ambazo ni sawa na 27, 174, 560 halafu wawe wanamkata katika mshahara wake.

Alisema, baada ya kupewa fedha hizo, kocha huyo alianza vituko na kushindwa kufanya kazi yake kwa mujibu wa mkataba wake, kitu kilichopelekea uongozi kukatisha mkataba wake. Alisema, kocha huyo alikuwa hana cha kuidai Simba kwa kuwa alikwishachukua fedha zake mapema baada ya kusaini mkataba.

Kocha huyo raia wa Croatia ameondoka nchini Jumanne usiku kwenda kwao. Hata hivyo, Rais wa Simba, Evans Aveva alikataa kulizungumzia suala hilo na kudai kuwa mkataba wa mwajiri na mwajiriwa ni siri.

Na mdadisiblog/festo saimon
 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

MKWASA AREJEA JIJINI DAR, ASUBIRI KUDAKA DILI JIPYA

Kocha maarufu nchini Charles Boniface Mkwasa amerejea nyumbani na kusema yuko huru kumfundisha timu yoyote inayomhitaji.

Mkwasa amerejea nyumbani baada ya mkataba wake na klabu ya Al Shaollah FC ya Saudi Arabia kuvunjwa ghafla. Mkwasa alikuwa msaidizi wa Hans van der Pluijm na wote mikataba yao ilivunjwa.

Akizungumza jijini Dar, kocha huyo na mchezaji wa zamani wa Yanga amesema yuko tayari ;kudaka’ kazi itakayojitokeza mbele yake. “Nimerejea nyumbani, nitapumzika kidogo ila kama kuna timu itanihitajia kuweza kufanya nao kazi sina tatizo katika hilo, tutafanya kikubwa ni maelewano,” alisema Mkwasa.

Aidha, Mkwasa alisisitiza lijifunza mengi licha ya kufanya kazi Saudi kwa kipindi kifupi.

Na mdadisiblog/festosaimon

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYEZA HAPA 

RONALDINHO ASHEREKEA MAMBO YAKE KWA KUTUNDIKA JEZI 78 ZIONE HAPA

RONALDINHO AMETUNDIKA JEZI ZAKE 78 KUSHEREKEA ALIKOPITA KISOKA. STAA HUYO ALIYEKUWA NA UWEZO WA JUU SANA, AMECHEZA TIMU KIBAO KWA MAFANIKIO. PAMOJA NA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL, BAADHI YA TIMU HIZO NI Gremio, through Paris Saint-Germain, Barcelona, Milan, Flamengo and, latterly, Atletico Mineiro

Na mdadisiblog/festo saimon
 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLIG HII ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

SIMBA YATUA KUANZA KAMBI ZANZIBAR BILA YA PHIRI

Simba imetua mjini Unguja tayari kuanza kambi ya kujiandaa na msimu mpya. Hata hivyo, kikosi cha Simba kimetua Zanzibar bila ya kocha wake, Patrick Phiri.

Selemani Matola ambaye ni kocha Msaidizi, ndiye atakiongoza kikosi hicho. Kwa mujibu wa uongozi wa Simba, Phiri ambaye juzi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Simba, atawasili Zanzibar leo kuendelea na kazi.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI MBALIMBALI PUNDE ZITUFIKIAPO