Saturday, August 16, 2014

LOGA AWAZIDI UJANJA SIMBA AJIPATIA MILIONI 27 NDANI YA WIKI TATU

ALIYEKUWA Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, amewazidi ujanja Simba baada ya kufanikiwa kujipatia sh. milioni 27 kwa muda wiki tatu.

Kocha huyo alianza kuinoa Simba mwishoni mwa mwaka jana alitokea timu ya Gor Mahia ya Kenya, kwa mkataba wa miezi sita, ambayo ilimalizika baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika. Hivi karibuni uongozi wa Simba uliamua kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja na kocha huyo, ambao ulidumu kwa wiki mbili kabla ya kusitishwa kwa ajira yake.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, zilieleza kuwa kocha huyo aliutaka uongozi uliopo madarakani kumpa Dola za Marekani 16,000, sawa na mshahara wa miezi minne. Mtoa habari huyo alisema, kocha huyo alikuwa analipwa dola za Marekani 5,000 sawa na Sh. milioni 8, 492 kwa mwezi, lakini kabla ya kusaini mkataba mpya aliwataka viongozi kumpa dola elfu 16 ambazo ni sawa na 27, 174, 560 halafu wawe wanamkata katika mshahara wake.

Alisema, baada ya kupewa fedha hizo, kocha huyo alianza vituko na kushindwa kufanya kazi yake kwa mujibu wa mkataba wake, kitu kilichopelekea uongozi kukatisha mkataba wake. Alisema, kocha huyo alikuwa hana cha kuidai Simba kwa kuwa alikwishachukua fedha zake mapema baada ya kusaini mkataba.

Kocha huyo raia wa Croatia ameondoka nchini Jumanne usiku kwenda kwao. Hata hivyo, Rais wa Simba, Evans Aveva alikataa kulizungumzia suala hilo na kudai kuwa mkataba wa mwajiri na mwajiriwa ni siri.

Na mdadisiblog/festo saimon
 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

0 comments:

Post a Comment