Saturday, October 11, 2014

TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ILIYOKUTANA OKTOBA 11, 2014- DAR ES SALAAM

KIKAO cha dharura cha Kamati ya Utendaji
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya
hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau wa
Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa
umma kama ifuatavyo: .

1.Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na
taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo
inaomba radhi kwa wadau ambao
wameguswa na kusumbuliwa na matukio
hayo.

2.Kufuatia matukio hayo, Sekretarieti ya TFF
kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua
mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi
ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe
wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau
wote waliohusika na upotoshaji huo
wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya
Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi
zao.

3.Kutokana na madai ya klabu kuhusu
vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu
2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga
kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu
siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili
kuwasikiliza na kushauriana kuhusu
changamoto za kikanuni na uendeshaji wa
mashindano kwa ujumla.

4.Kamati ya Utendaji itaendelea kuboresha
Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi
(Governing Regulations) ili kuweka uwiano
wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi
ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya
Utendaji itafanya kila linalowezekana
kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya
Ligi kwa lengo la kuwa na ligi
zinazoendeshwa kisasa (Professional
Leagues).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF).

0 comments:

Post a Comment