Thursday, October 02, 2014

RONALDO BADO BAO MOJA TU KUMKAMATA RAUL LIGI YA MABINGWA, MESSI ATUPWA HUKO!

BADO bao moja tu Cristiano Ronaldo afikie idadi ya mabao ya Raul anayeongoza kwa kufunga zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ronaldo usiku huu amezidi 'kuisuuza roho' ya kocha wake, Carlo Ancelotti baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad. Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti mara mbili dakika ya 11 na 25 kuipa ushindi Real Madrid. Mfalme wa mabao; Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebakiza bao moja kufikia rekodi ya Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Mwanasoka huyo bora wa dunia sasa anatomize mabao 70 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, moja nyuma ya Raul aliyefunga mara 71. Anafunga mabao hayo siku moja baada ya kocha Ancelotti kukaririwa akisema "Ni mchezaji bora zaidi niliyewahi kumfundisha,". Kipenzi huyo wa mashabiki wa Manchester United sasa anamzidi kwa mabao mawili, mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona, ambaye ana mabao 68. Ruud van Nisterlooy anashika nafasi ya nne kwa mabao yake 56, Thierry Henry mwenye mabao 50 ni wa tano, Alfred de Stefano mwenye mabao 49 ni wa sita, Andriy Shevchenko mwenye mabao 48 ni wa saba, wakati Eusebio mwenye mabao 46 sawa na Filippo Inzaghi wanashika nafasi ya nane. Didier Drogba anakamilisha orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa kwa mabao yake 42.

0 comments:

Post a Comment