Wednesday, October 01, 2014
|
KIUNGO Ander Herrera anatarajiwa kuwa nje
kwa wiki kadhaa baada ya kuchanika mbavu
akiichezea Manchester United dhidi ya West
Ham Jumamosi.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania
alimpisha Antonio Valencia baada ya kuumia
katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa
Old Trafford.
Taarifa iliyotolewa na United leo mchana
imesema: "Kiungo wa Manchester United,
Ander Herrera amechanika mbavu wakati wa
mechi na West Ham United Jumamosi.
Pichani Herrera akiwa ameshika ubavu wake wakati
akiondoka uwanjani Old Trafford baada ya
kuumia
"Mspanyola huyo alitolewa dakika ya 74 na
klabu hiyo itaendelea kuangalia hali yake
kwa karibu katika wiki kadhaa,".
Herrera anakuwa mchezaji wa tisa wa kikosi
cha kwanza cha Louis van Gaal kuwa nje ya
Uwanja kwa sababu ya maumivu na
wengine wakitumikia adhabu wakati
inajiandaa na mechi dhidi ya Everton
Jumapili.
Haifahamiki ni muda gani mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 25 atakuwa nje kwa
maumivu hayo, ambayo ni pigo lingine kwa
kocha wake.
Herrera amekuwa katika kiwango kizuri
United tangu ajiunge nayo kutoka Athletic
Bilbao mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Amecheza mechi za Ligi Kuu ya England
dhidi ya Swansea City, Queens Park
Rangers, Leicester City na West Ham.
Alifunga bao la pili la United katika ushindi
wa 4-0 dhidi ya QPR na akaifanya
United ionize 3-1 mbele ya Leicester, kabla
ya kufungwa 5-3. |
0 comments:
Post a Comment