Saturday, October 04, 2014
|
Jana ndio Waziri mkuu mpya wa Uganda
Ruhakana Rugunda kaapishwa ila kabla yake
alikua ni Amama Mbabazi ambae alifutwa kazi
wiki kadhaa zilizopita baada ya kukaa
madarakani toka May 2011 akitokea kwenye
Uwaziri wa Ulinzi.
September 18 2014 ndio Rais Museveni
alimuandikia Spika wa bunge barua kumuarifu
kuwa ameamua kumuondoa waziri mkuu huyo
na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekua Waziri
wa Afya ambae kwa sasa ana umri wa miaka
67. |
|
Kwa mujibu wa ripota wa TZA (millardayo.com
na AyoTV) waziri huyu alietimuliwa alikua
Waziri mkuu wa nne toka Rais Museveni aanze
kuitawala nchi hiyo January 1986 ambapo
mpaka sasa amewahi kuwa na Makamu wa
Rais wanaofikia wanne.
Picha zote hizi zinaonyesha wakati Serikali ya
Uganda ilipomnyang’anya ulinzi wa Wanajeshi
waziri huyu mkuu baada ya kufutwa kazi
ambapo kwenye hii picha ya chini anaeonekana
ni mke wake akilalamika kwa kutoamini
kilichotokea kwani mume wake na Rais
Museveni wamekua marafiki wakubwa.
Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti
kwamba kuna mambo mengi yaliyosababisha
kufutwa kazi kwa waziri huyu mkuu lakini
mambo hayo hayajawekwa wazi. |
|
Nyuma hii unayoiona ni nyumba anayoishi na
inayomilikiwa na Waziri huyu mkuu aliefutwa
kazi. |
Source millardayo
0 comments:
Post a Comment