Wednesday, October 01, 2014
|
CHELSEA imepata ushindi wa ugenini katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga
Sporting Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati
Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1
nyumbani na AS Roma ya Italia usiku huu.
Katika mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja
Matic dakika ya 34 limemfanya kocha Jose
Mourinho aitambie timu ya nchini kwake,
Sporting.
Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero alitangulia
kuifungia City kwa penalti dakika ya nne
kabla ya mkongwe Francesco Totti
kuisawazishia Roma dakika ya 23 katika
mchezo wa Kundi E.
Kocha Jose Mourinho kulia akimpongeza
Nemanja Matic baada ya kufunga bao pekee
la ushindi usiku huu
Bao pekee la Thomas Mueller dakika ya 22
limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0
ugenini dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi
katika mchezo mwingine wa Kundi E.
mchezo mwingine wa kundi hilo usiku huu,
Schalke 04 imelazimishwa sare ya 1-1
nyumbani na Maribor.
Kundi F, PSG imeichapa FC Barcelona
mabao 3-2, mabao yake yakitiwa kimiani na
David Luiz dakika ya 10, Marco Veratti
dakika ya 26 na Blaise Matuidi dakika ya 54,
wakati mabao ya wageni yalifungwa na
Lionel Messi dakika ya 12 na Neymar dakika
ya 56.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, APOEL
Nicosia imelazimishwa sare ya 1-1 na Ajax
nyumbani bao la wenyeji likifungwa na
Manduca dakika ya 31 na la wageni
likifungwa na Lucas Anderson mapema
dakika ya 28. |
|
Kundi H, BATE Borisov imeichapa 2-1
Athletic Bilbao nyumbani mabao ya washindi
yakifungwa na Denis Polyakov dakika ya 19
na Karnitskiy dakika ya 41, wakati bao la
wageni lilifungwa na Aritz Aduriz dakika ya
45.
Shakhtar Donetsk imelazimishwa sare ya
2-2 nyumbani na FC Porto, mabao ya
wenyeji yakifungwa na Alex Teixeira dakika
ya 52 na Luiz Adriano dakika ya 85, wakati
ya wageni yote yamefungwa na Jackson
Martinez dakika ya 89 kwa penalti na 90. |
0 comments:
Post a Comment