Sunday, September 14, 2014
 |
STRAIKA mahiri wa Simba, Mrundi Amissi
Tambwe, amesema alisikitishwa na taarifa za
kutaka kuchujwa kikosini kumpisha
mshambuliaji Emmanuel Okwi raia wa Uganda
na kuongeza kuwa anasubiri dirisha dogo la
usajili lifunguliwe ili afanye uamuzi mgumu.
Tambwe aliibuka kinara wa mabao msimu
uliopita lakini uongozi wa klabu hiyo ulikuwa
unafikiria kumchomoa kikosini hapo baada ya
kutakiwa kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni
kupisha usajili wa Okwi ili kukidhi idadi ya
wachezaji watano wa kigeni wanaoruhusiwa
kucheza katika klabu moja.
Simba tayari ilikuwa na Joseph Owino raia wa
Uganda, Donald Mosoti na Raphael Kiongera
raia wa Kenya pamoja na Warundi Pierre
Kwizera na Tambwe hivyo kutakiwa
kumpunguza mmoja. Mosoti ndiye aliyekuja
kuondolewa baadaye baada ya hoja ya Tambwe
kupata upinzani mzito.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Tambwe
alisema: “Najua kuwa mimi ndiye niliyekuwa
chaguo la kwanza la kuondolewa ili kumpisha
Okwi, nilisikitika sana nilipopata hizo taarifa
kwani tayari nilikuwa na mipango yangu mingi
niliyokuwa nimeiahirisha kwa ajili ya Simba.
“Siwezi kuweka wazi klabu nilizotaka kwenda
lakini nilikuwa na mipango mingi, kwa sasa
nasubiri dirisha dogo ili niweze kukamilisha
mipango yangu, mimi naifahamu kazi yangu na
huwa sichezi kwa kubahatisha,” alisema
Tambwe.
Hata hivyo straika huyo alisema: “Mosoti tayari
ameshaondoka, hakuna ujanja hao vijana
wanatakiwa wajitahidi kucheza kwa kuelewana
na kuisaidia timu, hapo tutasogea lakini ukweli
ni kwamba kuna vitu vya Mosoti ambavyo
tutavikosa.”credit mwanaspoti |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment