Sunday, September 14, 2014
 |
MANCHESTER, ENGLAND
KILA biashara ina masharti yake. Lakini
biashara ya Radamel Falcao kubaki jumla
Manchester United inaweza kuwa rahisi tu.
Masharti yake ni rahisi kuliko ya mganga wa
kienyeji.
Kwa mujibu wa habari za ndani za Old Trafford,
inadaiwa kuwa mkopo wa nyota huyo wa
kimataifa wa Colombia unaweza kuwa usajili wa
muda mrefu kama tu atafanikiwa kucheza
mechi 15 na kufunga mabao matano.
Akifanikiwa katika hilo, United italazimika
kutoa dau la Pauni 35 milioni huku ikimlipa
mshahara wa Pauni 11 milioni kwa mwaka
baada ya makato ya kodi, pia atajichotea kiasi
cha Pauni 2.4 milioni kama bonasi.
Falcao mwenyewe ana matumaini kuwa bodi ya
United itamchukua jumla baada ya mkopo
wake wa Pauni 6 milioni kutoka Monaco
ambao utaisha Juni mwakani. Juzi Alhamisi
alitambulishwa katika Uwanja wa Old Trafford
pamoja na kiungo Daley Blind aliyesajiliwa kwa
Pauni 14 milioni kutoka Ajax.
“Natumaini nitabakia Manchester United kwa
miaka mingi na kuweka historia katika klabu
hii. Nilipokuwa Porto na Atletico Madrid siku
zote nilipenda kuimarika na niliota kuchezea
klabu kama hii. Nataka kubaki hapa kwa miaka
mingi,” alisema Falcao.
“Naona kwa sasa klabu ipo katika kipindi
ambacho kila mmoja anataka kumjua
mwenzake. Lakini hapa kuna wachezaji wa hali
ya juu na wana akili sana na ambao wana
uwezo wa kufanya kile ambacho kocha anataka.
“Kuhusu suala la nitacheza wapi nadhani hilo ni
jambo ambalo kocha ataamua kwangu.
Nimekuwa na bahati ya kucheza katika klabu
kubwa duniani kote katika mechi kubwa na
fainali. Nimejikita katika kufurahia soka langu
na kutumia nafasi ambayo Manchester United
wamenipa.
“Siku zote huwa nina tabia ya kuweka malengo
yangu binafsi, hilo ndilo ambalo wachezaji
wanapaswa kujipa changamoto wenyewe.”
Staa huyo kwa msimu wa tano sasa
hajafanikiwa kucheza katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Falcao anatarajiwa kuvaa jezi ya Manchester
United kwa mara ya kwanza kesho Jumapili
katika pambano la Ligi Kuu England dhidi ya
QPR uwanjani Old Trafford. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment