ASHINDWA KUNG’ARA NANGWANDA
SIJAONA
Na Renatus Mahima, MTWARA
SIMBA SC imepata sare ya kwanza chini ya
kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya
kutoka 0-0 na Ndanda Uwanja wa
Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Katika mchezo huo, refa David Paul
aliyesaidiwa na Mohammed Kayanda na
Sawa Omar, wote wa hapa, timu zote
zilishambuliana kwa zamu vipindi vyote.
Jacob Masawe aliifungia bao Ndanda dakika
ya 51 ambalo hata hivyo, refa David Paul
alilikataa kwa kuwa mfungaji alikuwa
ameotea kabla ya kufunga, uamuzi ambao
haukuwaridhisha wenyeji.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais
wa Simba SC, aliyeongozana na Mwenyekiti
wa zamani wa klabu hiyo, mshambuliaji
Emmanuel Okwi alitokea benchi dakika ya
60 kuchukua nafasi ya Abdallah Seseme,
lakini hakuonyesha cheche zake.
Huo unakuwa mchezo wa sita kwa Phiri
tangu arejee Simba SC mwezi uliopita,
akirithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko
Logarusic baada ya awali kushinda 2-1 na
Kilimani City, 2-0 na Mafunzo, 5-0 na
KMKM, 3-0 na Gor Mahia na kufungwa 1-0
na URA.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Hussein
Sharrif ‘Cassilas’, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Abdi Banda, Abdul Azizi, Joram Mgevege,
Said Ndemla, Ibrahim Twaha, Amisi
Tambwe, Abdallah Seseme, Ibrahm Ajibu,
Ramadhani Singano ‘Messi’.
Ndanda; Salehe Malande, Shukuru
Chachala, Paul Ngalema, Ernest Joseph,
Cassian Ponela, Amir Msumi, Jacob
Masawe, Hamisi Salehe, Omar Nyenge,
Gideon Benson, Nassor Kapama. |
0 comments:
Post a Comment