Friday, September 19, 2014

HUYU NDO MCHUNGAJI ALIYETEKA ROHO ZA WENGI NIGERIA

Marais wengi Afrika wamemtembea Joshua wakitafuta kuombewa Kanisa lililoporomoka mjini Lagos wiki jana , na kuwaua watu wengi, lilikuwa linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB Joshua. Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu na waathiriwa wa HIV. TB Joshua anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia ya MH370" Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia. Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini, akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15. Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake manabii wakimtaka kuhubiri na kufanya miujiza.

0 comments:

Post a Comment