Saturday, September 20, 2014
|
KUITWA KUHOJIWA
Home » Unlabelled » HUJUMA STARS,
TFF KUUNDA JOPO LA KUCHUNGUZA,
VIGOGO KUITWA KUHOJIWA
Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)
limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa
zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya
Habari zikielezea tuhuma za hujuma kwa
timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za
kufuzu mashindano ya AFCON.
TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa
tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya.
TFF itateua jopo la kuchunguza tuhuma hizi.
Wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania
(Members of TFF Family) watakaohitajika
kuhojiwa na jopo hilo kwa mujibu wa Ibara
ya 37 ya Kanuni za Maadili za TFF
watalazimika kutoa ushirikiano.
Atakayeshindwa kutoa ushirikiano
atachukuliwa hatua za kimaadili.
Pia wadau wa mpira wa miguu ambao sio
wanafamilia wa TFF, watakaoitwa na jopo
hili wanaombwa watoe ushirikiano kwa nia
ya kujenga mpira wetu. |
0 comments:
Post a Comment