Friday, September 19, 2014
 |
| KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba
Diego Costa hawezi kucheza mechi tatu kwa
wiki Chelsea kwa ababu ya maumivu ya
nyama aliyoyapata akiitumikia timu yake ya
taifa, Hispania.
Costa, ambaye amefunga mabao saba katika
mechi zane nne za awali Chelsea, alilazimika
kuanzia benchi katika mchezo wa sare ya
1-1 na Schalke Ligi ya Mabingwa Ulaya
usiku wa jana.
Pamoja na hayo, Mourinho hakuwa na
malalamiko coyote kwa Hispania zaidi ya
kusema na wao pia wanamhudumia vizuri
mshambuliaji huyo juu matatizo yake ya
misuli yanayomkabili. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment