Friday, September 19, 2014

MCHAMBUZI WA SOKA MAHARUFU DUNIANI ATABIRI MATOKEO YA MECHI KATI YA MANCHESTER CITY vs CHELSEA

Ligi kuu ya Uingereza inataraji kuendelea wikiendi hii kwa michezo ya mzunguko wa tano huku klabu ya Chelsea ikiwa bado inaongoza msimamo wa ligi hiyo wakati Newcastle United ikishika mkia. Mchambuzi mahiri wa soka kutoka nchini Uingereza,Paul Merson anakuja kwa mara nyingine na ubashiri wake wa mchezo wa chelsea na manchester cty Ambapo amesema matokeo yatakua 1-1 iwapo diego Costar atacheza mchezo huoMchambuzi huyo alisisitiza kwamba iwapo mshambuliaji mahiri wa Chelsea,Diego Costa hatocheza Jumapili kutokana na majeraha ya nyama za paja aliyoyapata tangu wiki iliyopita kwenye timu yake ya Taifa ya Uhispania basi Man City wataibuka na ushindi wa goli 2-0. Licha ya nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid kusumbuliwa na maumivu ya kuchanika nyama za paja lakini Jose Mourinho amezidi kumpanga mchezaji huyo anayeongoza kwa upachikaji wa mabao akiwa amefunga magoli saba mpaka sasa. Na mdadisiblog/festosaimon

Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment