Saturday, September 27, 2014
 |
Ukishangaa ya usiyemjua,
utayaona ya TFF. Sasa
imeibuka na jipya na
kutaka Yanga, Simba na
klabu nyingine 12 za Ligi
Kuu Bara, zikatwe 5% ya
fedha za udhamini, ziingie
TFF.
Uongozi wa TFF umeandika
barua kwenye bodi ya ligi
ukitaka ulipwe 5% ya
fedha za udhamini kutoka
Vodacom na Azam TV ipewe
yenyewe.
TFF imetaka fedha hizo ili
izitumie kwa ajili ya
maendeleo ya soka au timu
ya taifa.
Lakini hali imezishitua
baadhi ya klabu ambazo
zimeanza kuhoji chinichini
kuhusiana na suala hilo.
Suala hilo la kushangaza
kama litapita litakuwa ni
la aina yake kwa klabu
kutoa fedha zao za
udhamini na kulipa
shirikisho.
Suala hilo ambalo
limeonekana litakuwa la
kwanza kufanyika katika
ulimwengu wa soka, bado
haijajulikana kama
limepitishwa.
Barua hiyo ya Septemba 19
kutoka TFF ikiwa
imesainiwa na Katibu Mkuu,
Mwesigwa Celestine,
imeitaka bodi ya ligi
kupeleka fedha hizo za
klabu 14 za ligi kuu
kwenye akaunti ya
shirikisho hilo.
TFF imesema fedha hizo
zitaenda kwenye akaunt ya
Maendeleo ya Michezo
Tanzania ambayo
hushughulikia timu ya
taifa.
(Kimantiki Vodacom na Azam
TV hazidhamini timu ya
taifa, inadhaminiwa na
Kilimanjaro Beer.) |
0 comments:
Post a Comment