Waziri wa Ulinzi nchini Ukraine amesema kuwa mojawapo ya ndege zake za kijeshi kubeba mizigo imedunguliwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Luhansk mashariki mwa taifa hilo.
Ndege hiyo ya jeshi la j la Ukraine ilikuwa ikiwabeba wanajeshi pamoja na vifaa. Ripoti zinaarifu kuwa wafanyakazi wa ndege hiyo pamoja na wajeshi wote 49 wamefariki.
Idara ya maswala ya kigeni mjini Washington ,Marekani imesema kuwa ina hakika kwamba mizinga pamoja na silaha nyengine kali zinazomilikiwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga nchini Ukraine zilitoka nchini Urusi.
Msemaji wa Idara hiyo amesema kuwa mizinga iliokuwa katika kambi moja ya silaha za kijeshi kusini magharibi mwa Urusi iliondolewa katika kambi hiyo.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza Hague amesema kuwa kuingia kwa vifaa hivyo nchini Ukraine hakuwezi kukubalika.
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment