KIUNGO, Mkenya Humphrey Mieno amesema kuwa usajili uliofanywa na timu yake ya zamani ya Azam kuwachukua kiungo Frank Domayo na Didier Kavumbagu utawasaidia kufanya vizuri msimu ujao na kupoteza " wa Simba na Yanga.
Mieno ambaye kwa sasa anacheza klabu ya Sofapaka ya Kenya alisema; “Azam wamefanya usajili mzuri sana kwa kumchukua Domayo na Kavumbugu kutoka Yanga, naamini Simba na Yanga kwa sasa zina wakati mgumu kupambana na Azam tena naona kuwa msimu ujao utakuwa wa Azam pia”“Azam wamesajili vizuri.
Kiungo ambaye nilikuwa namkubali zaidi nilipokuwa nacheza Tanzania alikuwa ni Frank Domayo kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi zinazosababisha mabao.
Hapondipo nilipomwona akiwa na utofauti mkubwa na Sure Boy (Salum Aboubakari) na hata Kipre Bolou.“Sure Boy namkubali sana kwa kupiga pasi nyingi na kuzunguka kila kona ya uwanja, Bolou anapiga pasi za kupandisha mashambulizi,” alisema Mieno.
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment