Monday, May 12, 2014

KISHAELEWEKA TAYARI JANGWANI MBUYU TWITTE AONGEZA MKATABA YANGA

Beki kiraka wa Yanga sport club Mbuyu Twitte leo ameongoza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia yanga baada ya kukubaliana na uongozi na kupata majibu ya ya shikisho la soka la Tanzania (TFF) kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni msimu wa mwaka 2014/2014.

Usajili wa twite umefanyika leo makao makuu chini ya katibu mkuu Ben Njovu. Ambapo mbuyu twitte amehaidi kuendelea kujitolea kuisaidia timu ya Yanga.

Akiongea Twitte amesema ana furaha kuendelea kuitumikia yanga kwani anafurahia maisha ya Jangwani kwani wapenzi,viongozi na wachezaji ni marafiki ndani na nje  ya uwanja.

Aidha amesema kuwa timu ya Yanga ni timu kubwa Barani ulaya na inawanachama  wengi ivo najisikia vizuri kuendelea kuitumikia yanga.

Mbuyu twite ameitumikia Yanga tangu juni 2012 aliposajiliwa huku akiwa katika kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliisaidia Yanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu.
Source : jombii man

Posted by festo saimon

Posted by festo saimon


Posted by festo saimon

0 comments:

Post a Comment