Tuesday, August 12, 2014

MBEYA YAKIONA CHA MOTO KWA WATOTO WA TMK AIRTEL RISING STARS

TIMU ya wavulana ya Temeke jana imeyaanza vyema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwa kuifunga Mbeya 2-1 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa kumbu kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Baada ya kosa kosa za hapo na pale kutoka pande zote mbili, Temeke walifanikiwa kuandika bao lao la kwanza katika dakika ya 27 kupitika kwa mshambuliaji machachali Siaba Selehe.

Bao hilo lilipokelewa kwa nderemo na vifijo na mashabiki wa Temeke. Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira na kipa wa timu ya vijana ya Mbeya, Kelvin Dismas (kulia) na beki Yusufu Hongoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila upande ukitafuta goli na Mbeya waliweza kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Mantony Malewa aliyefanya kazi ya ziada kupangua ngome ya Temeke na kuweka mpira kimiani.

Goli hilo liliongeza kasi ya mchezo huku Temeke wakisaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 70 kupitia kwa Said Mussa.

Katika mechi ya wasichana ya fungua dimba ya wasichana, timu ya Ilala ilifanya mauji ya kuungamiza baada ya kuifunga Mwanza 6-0. Dalili za kupoteza mchezo huo kwa vijana wa Mwanza ilianza kuonekana mapema ambapo Ilala walipata goli la kwanza katika dakika ya sita kupitia kwa Rehema Abdul ambaye alifunga manne peke yake.

Abdul alifunga magoli mengine katika dakika za 38, 47 na 67 huko magoli megine yakigungwa na Arasa Abdul katika dakika za 56 na 65. Kwa ujumla Ilala walitawala mchezo katika kila idara.

Mechi nyingine zilizotarajiwa kuchezwa jana ni kati ya Zanzibar na Temeke (wasichana) na Ilala dhidi ya Mwanza (Wavulana). Mashindano hayo ya kubaina na kuendeleza vipaji ngazi ya Taifa yalitarajiwa kufunguliwa rasmi na Mjumbe wa Heshima wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) Said El Maamry.

Wachezaji 32 watachaguliwa katika mashindano haya ili kuunda timu za wasichana na wavulana ili kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars itakayofanyika nchini Gabon baadaye mwezi huu.

 HABARI ZINGINE ZIPO HAPA BONYA UZIONE 

KOCHA KIBOKO YA YANGA AWASILI DAR KUMWAGA WINO NA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM KOCHA bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam Ijumaa wiki hii kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC.

Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi. Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Mazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Phiri na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi. Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji. Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.

Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

Simba SC juzu ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.

Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

 KAMA UNATAKA KILA HABARI NIKIPATA ZIKUFIKIE KIRAHISI BONYA HAPA 

JE NIKWELI JOKATE ANAPENDA KUIGA MASTAA WA MAMTONI?!!! CHEKI PICHA HIZI

Urembo ni kitu kizuri na kwenda na Fasheni ndio msingi wakuonekana HOT kila wakati...mwanadada Jokate hayuko nyuma kwenda sambamba na wakali wa nje...big up!!!...umeziona  picha hizo  ni kwajinsigani anavyokwenda nao kwenye upande wa NYWELE!!!

PICHA ZA WEMA NA DIAMOND WAKILA GOOD TIME ZIWANI JIJINI MWANZA!!!

Monday, August 11, 2014

Umesikia alichokisema Mke wa Dansa wa Diamond kuhusu anti Ezekiel?kipo hapa.

Wiki iliyopita alisikika Anti Ezekiel akielezea uhusiano wake na Moses Iyobo ambaye ni dansa wa Diamond Platnumz,sasa leo amesikika mpenzi wake ambaye ndiye anaishi nae ambaye kaongea na Soud Brown kuhusu hili jambo. BONYEZA HAPA KUSIKILIZA 

Source millardayo

SIMBA SC YAWAPA MIKATABA YA MIAKA MIWILI KILA MMOJA , KWIZERA NA KIONGERA...SASA ‘MAPROO’ WAMETIMIA MSIMBAZI

Wanaungana tena; Paul Kiongera alicheza pamoja na Donald Mosoti Gor Mahia ya Kenya

SIKU moja baada ya kuvunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic, Simba SC imewasainisha mikataba ya miaka miwili kila mmoja, kiungo Pierre Kwizera raia wa Burundi na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera.

Simba SC jana ilivunja mkataba na Loga ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakaimu Ukocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Wawili hao wanakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni katika klabu hiyo kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiungana na mabeki Mganda Joseph Owino, Mkenya Donald Mosoti na mshambuliaji Mrundi, Amisi Tambwe.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane. Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

RASMI, MANGALA NI MCHEZAJI WA MANCHESTER CITY, AKAMILISHA KILA KITU

KLABU ya Manchester City imethibitisha kukamilisha usajili wa Eliaquim Mangala kutoka Porto, na mchezaji huyo amesema anataka kushinda mataji na mabingwa hao wa England.

Man City ambayo inakamilisha usajili wa mchezaji huyo siku moja baada ya kufungwa na Arsenal mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii, inaaminika wamelipa Pauni Milioni 32 kumpata mchezaji huyo.

Beki huyo wa kati atavaa jezi namba 20 Uwanja wa Etihad, na pia amesema kusajiliwa kwa mchezaji mwenzake wa Porto, Fernando Man City kumesaidia.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

KUMBE MANYAUNYAU NI TAPELI: SHAHIDI AELEZEA JINSI WALIVYOTAPELIWA SH 29.6 MIL NA MGANGA HUYO

Dar es Salaam, Shahidi wa pili katika kesi ya kujipatia Sh29.6 milioni kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa jadi, Dunia Salumu (37) ‘Manyaunyau’ amedai kuwa walilazimika kuuza kiwanja na nyumba ya urithi kutafuta fedha za kununua mabeberu saba na mafuta ya ngamia ili kumpa mganga huyo kama masharti ya kumfufua ndugu yao aliyefariki dunia.

Manyaunyau alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Desemba mwaka 2013 akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha hizo kutoka kwa Tecla Modest.

Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Nassoro Katuda shahidi huyo, Diana Steven (26) alidai kuwa baada ya kumaliza matanga ya mjomba wake, Saimon Modest aliyefariki mwaka 2008, wakiwa nyumbani Mchikichini, Dar es Salaam walisikia sauti ya mtu ikisema kuwa ‘mimi sijafa’.

Wakati Diana akiendelea kutoa ushahidi huo mrefu, Hakimu Wilberforce Luhwago, alimkatisha akieleza kuwa ameisikiliza kesi hiyo kwa muda mrefu na kuna nyingine za kusikiliza, hivyo itaendelea Agosti 13, mwaka huu.

Ushahidi wenyewe

Alisema siku tatu baada ya mazishi ya mjomba wake, ndugu yao aitwaye Hamisi akiwa na Manyaunyau walifika nyumbani kutoa pole na walipofika Manyaunyau alidai kuwa marehemu hajafa, bali ameuawa na kaka yake na amechukuliwa na Mpemba kwa ajili ya kwenda kuuza duka.

“Mimi na mama zangu wawili tulishtushwa na kuhoji, mtu aliyekufa anaweza akawa hai?” alisema Diana katika ushahidi wake uliochukua saa nane.

“Baada ya hapo alituambia siku iliyofuata twende ofisini kwake (Manyaunyau), Mburahati, tukiwa na Sh100,000. Mama zangu walisema hawana, lakini ndugu yetu mmoja aitwaye Bright Steven alikwenda kwenye ATM na kuchukua Sh80,000 na safari ikafanikiwa,” alidai.

Diana alisema baada ya kupeleka fedha hizo, Manyaunyau aliwapangia kwenda siku nyingine, akiwataka kurudi wakiwa na kitambaa cheusi na walipokipeleka alisema alikichukua na kukifunika kikaanza kutoa sauti ya mtu mzima ikisema: “Karibuni sana wajukuu zangu na maelezo yote mtapewa na mwenyeji wenu.”

Alisema Manyaunyau pia aliwataka wapeleke chupa sita za mafuta ya ngamia wakiyakosa wampelekee Sh1.8 milioni. Alisema walimpelekea fedha hizo walizozipata kwa kuuza sehemu ya kiwanja walichorithi kwa mama yao.

“Siku tuliyopeleka hiyo hela pia tulipeleka mtama, jogoo mwekundu na tulipelekwa katika pori lililopo Kibamba na kila tulipokuwa tukienda kule Kibamba tulikuwa tunakodi teksi kwa Sh40,000,” alidai Diana.

Alidai kuwa kabla ya kufika katika pori hilo, Manyaunyau aliwaagizia soda wakanywa na baada ya kumaliza aliwaambia wapige makofi huku wakisema hodi hodi mkubwa!

“Tuliingia katika pori hilo saa 2: 00 usiku, tukaona mwanga kama radi imepiga na tukaona kitu cheupe kama mtu kafunikwa sanda... ile tuliyoipeleka kwa Manyaunyau siku chache kabla ya kwenda katika pori hilo.

“Alituambia mtu wenu ndiyo huyo ila msimfunue kwa sababu ni mchafu, akasema inatakiwa hela ya kununua mafungu mawili ya dawa ya kumsafishia.

Sisi hatukuelewa, ndipo alipotuambia siku iliyofuata twende ofisini kwake atufafanulie. Tulipofika alituambia anataka mbuzi saba madume na Sh2 milioni na kwenda naye tena Kibamba.

“Tukiwa porini hapo tulisikia sauti ya babu ikisema marehemu wenu ameshikiliwa na wachawi, wanataka damu ya mbuzi saba, hivyo tulirudi nyumbani na kwenda kuuza tena kiwanja kilekile kwa mtu mwingine na kupata Sh4.9 milioni na kuzipeleka kwa Manyaunyau kununulia mbuzi hao,” shahidi alidai na kuongeza kuwa ‘babu’ alizidi kuongeza madai, mara hii akisema anataka nguo, mkeka na chakula nyumbani kwa Manyaunyau.

“Baada ya kauli ya babu, tulipeleka chakula kwa Manyaunyau na hapo alituambia tujiandae kwa safari ya Majohe na huko tulikwenda mimi na mama zangu wawili na mke wa Manyaunyau na tulipofika tuliongea tena na ‘babu’ na kutuambia tutafute Sh2 milioni nyingine kwa ajili ya kumkomboa ndugu yetu.”

Waliporudi kutoka Majohe, alidai kuwa walikwenda kukopa kwa riba na Manyaunyau alisema fedha hizo wazifunge katika kitambaa cheusi na kuziweka katika ndoo na kuzipeleka katika Msitu wa Majohe.

“Tulipofika Majohe tulipiga makofi na kuziweka zile pesa na siku iliyofuata Manyaunyau alituambia tutoe Sh3.5 milioni kwa ajili ya kukanyagia na sisi tulizipelekea hukohuko Majohe.”

Alidai kuwa siku iliyofuata walikwenda ofisini kwa Manyaunyau na kuambiwa kuwa wapeleke chakula nyumbani kwake baada ya hapo waende kumwangalia mchawi aliyemchukua ndugu yao huko Kibamba eneo la makaburi.

“Tulipofika eneo hilo la makaburi alitokea mtu mrefu sana akiwa ameshikilia mkia na akapiga magoti na hapo hapo alitokea tena mtu mnene na kusema hamuwezi kumuona ndugu yenu kwa sasa.”

Diana alidai kuwa baada ya kuambiwa hivyo, ilisikika sauti ya ‘babu’ ikisema watafute Sh5 milioni nyingine.

“Tulivyosikia hiyo sauti ya ‘babu’ akisema tutafute ndugu zangu walisema hawana hiyo hela na sauti ya babu iliendelea kusema kuwa nyie leteni tu hiyo hela marehemu akija atailipa,” alieleza.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

NEW UPDATES: UNDANI ZAIDI WA KIBONDE WA CLOUDS FM ALIVYOTIWA MBARONI!

Mtangazaji Ephraim Kibonde akidhibitiwa na Polisi wa usalama barabarani maeneo ya Mwenge.

WIKIENDI iliyopita haikuwa njema kwa mtangazaji Ephraim Kibonde baada ya kutupwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa msala wa kudaiwa kugonga gari na kutoa lugha ya matusi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho ambapo gari alilokuwa akilitumia Kibonde, liligonga kwa nyuma gari jingine na kisha kukimbia.

“Baada ya kugonga, Kibonde alirudi nyuma kisha kuanza kukimbia ambapo trafiki alitumia gari lililogongwa na Kibonde kumkimbiza,” kilimwaga data chanzo hicho.

Chanzo hicho kilifafanua kuwa baada ya polisi kumkimbiza kwa saa kadhaa, walifanikiwa kumkamata maeneo ya Mwenge ambapo trafiki alipanda kwenye gari la Kibonde na kumuamuru arudi eneo la tukio lakini Kibonde hakuwa tayari kurudi ndipo alipoanza kukimbia tena, huku askari aliyemkamata akiwa ndani ya gari.

“Inaonekana kulitokea kutoelewana kati ya askari na Kibonde ndipo askari huyo alipowasiliana na wenzie kwa njia ya radio call ili wambananishe na alipofika Ubungo kwenye mataa wakamtaiti na kumpeleka kituoni, Oysterbay,” kilihitimisha chanzo chetu.

Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alitia timu katika kituo cha Oysterbay ili kutaka kujua mustakabali mzima wa ishu hiyo ambapo alimshuhudia Kibonde akiwa amesimama nyuma ya nondo huku akiwa anaimba ‘nyimbo’ anazozijua mwenyewe.

Mtangazaji huyo amefunguliwa kesi iliyopewa RB namba OB/RB/13806/20014 KUGONGA NA   LUGHA YA MATUSI.

 USIPITWE TENA NA HABARI ZETU KWA KUBONYEZA HAPA ILI UHUNGANE NASI 

KAULI YA ASKOFU KAKOBE MARA BAADA YA GWAJIMA KUNUNUA HELKOPTA

Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.

Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’ ‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ –

Kakobe Kuhusu Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu, mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana

 KAMA UNATAKA USIPITWE NA HABARI PUNDE NIZIWEKAPO MTANDAONI BONYA HAPA 

New AUDIO | AT - Sitaki Kusemwa | Download hapa

New AUDIO | MKUBWA NA WANAWE - NISEME | Download hapa

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA ZIPO HAPA

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express), Borussia Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na Arsenal, Liverpool na Manchester United (Metro), Manchester City wapo karibu kukamilisha usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23 kwa kitita cha pauni milioni 32 (Daily Mail), beki wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno, 22, atakamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool wiki ijayo, baada ya kucheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Real Madrid katika michuano ya Uefa Super Cup, jijini Cardiff (Daily Mirror), Atletico Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Roberto Soldado, 29, kwa mkopo, lakini Spurs wangependa kumuuza kabisa (Daily Telegraph), Tottenham wanamfuatilia winga kutoka Nigeria Moses Simon, 19 anayechezea Trencin (Daily Mirror), Everton wamekubaliana na Chelsea kumchukua Christian Atsu, 22 kwa mkopo (Daily Mail), Real Madrid wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumchukua kipa, Petr Cech (Daily Express), wakala wa winga wa Fiorentina Juan Cuadrado atasafiri kwenda England weekend hii ili kuzungumza na Manchester United juu ya mkataba wa pauni kati ya milioni 30 hadi 35 (Marca), Liverpool watamfuatilia Ezequiel Lavezzi baada ya PSG kumwambia mshambuliaji huyo kuwa atauzwa (Daily Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

 JIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

JE WAJUA KUA NEY NDO CHANZO CHA DIAMOND KUHAIRISHA KUMUOA WEMA??? SOMA CHANZO HAPA

IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki.

Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Ushauri huo umekuwa mwiba kwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu ambaye amekuwa na ndoto ya kuolewa na staa huyo anayekimbiza kitaani na wimbo wake wa Mdogomdogo.

Akifafanua zaidi kuhusiana na ushauri huo, Nay alisema: “Kuna mifano mingi sana nimeiona kutoka kwa wasanii ambao wameoa, wengi wao wameshasanda sasa mdogo wangu (Diamond) na yeye alipoleta hoja ya kutaka kuoa nikaona sasa anatafuta shimo la kwenda kujifukia, nikamshauri aache.”

CREDIT : GPL

 HABARI ZINGINE ZIPO HAPA BONYA UZISOME 

AZAM FC YAIWAKILISHA VYEMA YANGA KAGAME, WAIFUMUA KMKM 4-0 AMAHORO

Kikosi cha Azam FC kilichoua 4-0 leo Kombe la Kagame

AZAM FC waliochukua nafasi ya Yanga SC kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, jana wameifumua KMKM ya Zanziabr mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A, Uwanja wa Amahoro, Kigali.

Azam FC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 3-0, mawili akifunga mshambuliaji wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint Preux na lingine Nahodha John Bocco. Adebayor.

Alianza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Bocco au Adebayor aliyefunga bao la kwanza dakika ya kwanza tu kabla Leonel kufunga mara mbili mfululizo dakika za 18 na 29. Kipindi cha pili, Azam FC walitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini walifanikiwa kufunga moja tu, Bocco tena daika ya 52.

Kocha Mcameroon Joseph Marious Omog aliwapumzisha Bocco, Kipre Herman Tchetche na David Mwantika kipindi cha pili na nafasi zao kuchukuliwa na Khamis Mcha ‘Vialli’, Didier Kavumbangu na Said Mourad.

Vialli na Kavumbangu walikwenda kuongeza kasi ya mashambulizi ya Azam FC, lakini safi ya ulinzi KMKm ilisimama imara kukataa kuruhusu mabao zaidi.

Azam FC sasa inafikisha pointi nne baada ya awali kutoa sare ya bila kufungana na wenyeji Rayon katika mchezo wa kwanza, wakati KMKM na timu nyingine zote zina pointi moja kila moja.

Azam FC: Mwadini Ally, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika/Said Mourad (dk 47), Aggrey Moris, Boluo Michael, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sureboy’, Kipre Tchetche/Didier Kavumbangu dk11, Lionel Saint Preux na John Bocco/Khamis Mcha dk65. KMKM: Mudathir Khamis, Khamis Ali, Pandu Hajji, Makame Mngwali, Mwinyi Mngwali, Ibrahim Khatib, Ameir Khamis/Iddi Kambi dk84, Moka Msafiri/Haji Salim (dk 24), Juma Faki, Mudrik Abdullah na Maulid Ramadhani

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

SABABU ZA SIMBA SC KUACHANA NA LOGA HIZI HAPA

LIVERPOOL YAWAFUMUA BORUSSIA DORTMUND 4-0

Mfungaji wa bao la kwanza la Liverpool, Daniel Sturridge akishangilia

LIVERPOOL imeonyesha inayaweza kabisa maisha bila Luis Suarez baada ya kuifumua mabao 4-0 Borussia Dortmund katika mchezo wa mwisho wa kujiandaa na msimu Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Daniel Sturridge dakika ya 10, Dejan Lovren dakika ya 14, Phillippe Coutinho dakika ya 49 na Jordan Henderson dakika ya 61.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet; Manquillo/Kelly dk85, Johnson/Enrique dk61, Skrtel, Lovren; Gerrard, Can/Lucas dk46, Henderson/Allen dk80, Sterling, Coutinho/Ibe dk72 na Sturridge/Lambert dk76. Borussia Dortmund: Langerak; Piszczek/ Großkreutz dk58, Sokratis/Knystock dk81, Ginter, Schmelzer/Sarr dk81, Kehl/Bender dk46, Kirch/Immobile dk46, Mkhitaryan/Ji dk64, Aubameyang/Bandowski dk76, Jojic/ Amini dk77 na Ramos/Hofmann dk46.

 HABARI NYINGINE BONYEZA HAPA KUZISOMA 

AS VITA NA TP MAZEMBE ZOTE ZATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

KLABU ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Zamalek FC ya Misri.

Kwa matokeo hayo, wameungana na wapinzani wao wakubwa, TP Mazembe ya DRC pia, ambayo wameifunga Al Hilal ya Sudan mabao 3-1 mjini Lubumbashi jana pia.

Zamalek walishindwa kufurukuta kwenye Uwanja wa nyumbani wa Alexandria, wakikubali bao la wageni dakika ya 54 lililofungwa na kinda wa Uganda, Yunus Junior Ssentamu.

Ushindi huo unaifanya AS Vita itimize pointi 10, nyuma ya TP Mazembe, wenye pointi kama hizo na wastani mzuri zaidi wa mabao.

Hilo apo juu  lilikuwa bao la kwanza la Ssentamu katika Ligi ya Mabingwa akiwa na AS Vita aliyojiunga nayo miezi miwili iliyopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa SC Vipers ya Ugandan alisajiliwa baada ya kuifungia mabao matatu Uganda Cranes katika CHAN mwaka 2014 nchini Afrika Kusini. AS Vita sasa watacheza mechi ya mwisho na mahasimu wao, TP Mazembe kuamua timu ya kupaa kileleni kwa Kundi A, wakati Zamalek watasafiri hadi Khartoum, Sudan, kuwafuata Al Hilal katika mechi ya kukamilisha ratiba.

Katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, wenye walipata mabao yao kupitia kwa Rainford Kalaba, Solomon Asante na Adama Traore baada ya kazi nzuri ya Mtanzania, Mbwana Samatta.

Bao pekee la Hilal lilifungwa na mkongwe wa Sudan, Mudather El Tahir.

 STORY NYINGINE BONYEZA HAPA KUZISOMA 

FABREGAS AFUNGA BAO LA USHINDI CHELSEA

Mfungaji wa bao la ushindi la Chelsea leo, Fabregas akishangilia

USHINDI CHELSEA CHELSEA imeshinda mabao 2-1 katika mchezo wake wa mwisho wa kujiandaa na msimu dhidi ya Ferencvaros nchini Hungary. Wenyeji walitangulia kupata bao kupitia kwa Gera dakika ya 17, kabla ya Ramires kuisawazishia timu ya Mourinho dakika ya 51 na Fabregas kufunga la ushindi dakika ya 81.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech/Schwarzer dk46, Azpilicueta/Moses dk60, Christensen/ Cahill dk46, Zouma/Ake dk75, Luis/Ivanovic dk46, Mikel/Hazard dk46, Ramires/Matic dk61, Schurrle/Salah dk46/Van Ginkel dk79, Willian/Fabregas dk46, Torres/Costa dk46 na Drogba/Oscar dk28.

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

PICHA KAMILI UZINDUZI WA ALBUM YA KAMATA PINDO LA YESU YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR ES SALAAM

Mgeni rasmi akimkabidhi Msama ahadi yake ya kununulia CD
Mama Sumaye, Rose na Baba Sumaye
Meza kuu ikiwa imesheheni.
Glorious worship Team wakiwa jukwaani.
Mwanamama Upendo Kilahiro hakuwa nyuma kuziangusha ngome za shetani katika uzinduzi huo.
Jessica BM akipunga mkono kwa furaha.
Ni ngumu kuketi wakati Rose anaiimba, lakini pia ilikuwa ngumu zaidi kwa Emanuel Mbasha kutofika jukwaani.
Mgeni rasmi mheshimiwa Fredrick Sumaye wakati anaingia ukumbini.
Haya sasa mambo yalinoga zaidi kama uonavyo.
Jessica BM na kundi lake wakimsifu Mungu.
Mheshimiwa Sumaye akisalimiana na Rose Muhando.
Jessica wa Boniphace Magupa. (mtu na mkewe
Kamata Pindo ikiwa hewani.
Wengine wanapongeza kwa hela/mshiko/ ankara, jamaa akaamua kumbeba huyu.
Ephraim Sekeleti kutoka Zambia hakuwa nyuma katika uzinduzi huo.
Baadhi ya umati wa watu waliohduhuria uzinduzi huo.

Source GK

 STORY NYINGINE SOMA HAPA BONYA