KLABU ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Zamalek FC ya Misri.
Kwa matokeo hayo, wameungana na wapinzani wao wakubwa, TP Mazembe ya DRC pia, ambayo wameifunga Al Hilal ya Sudan mabao 3-1 mjini Lubumbashi jana pia.
Zamalek walishindwa kufurukuta kwenye Uwanja wa nyumbani wa Alexandria, wakikubali bao la wageni dakika ya 54 lililofungwa na kinda wa Uganda, Yunus Junior Ssentamu.
Ushindi huo unaifanya AS Vita itimize pointi 10, nyuma ya TP Mazembe, wenye pointi kama hizo na wastani mzuri zaidi wa mabao.
Hilo apo juu lilikuwa bao la kwanza la Ssentamu katika Ligi ya Mabingwa akiwa na AS Vita aliyojiunga nayo miezi miwili iliyopita.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa SC Vipers ya Ugandan alisajiliwa baada ya kuifungia mabao matatu Uganda Cranes katika CHAN mwaka 2014 nchini Afrika Kusini. AS Vita sasa watacheza mechi ya mwisho na mahasimu wao, TP Mazembe kuamua timu ya kupaa kileleni kwa Kundi A, wakati Zamalek watasafiri hadi Khartoum, Sudan, kuwafuata Al Hilal katika mechi ya kukamilisha ratiba.
Katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, wenye walipata mabao yao kupitia kwa Rainford Kalaba, Solomon Asante na Adama Traore baada ya kazi nzuri ya Mtanzania, Mbwana Samatta.
Bao pekee la Hilal lilifungwa na mkongwe wa Sudan, Mudather El Tahir.
0 comments:
Post a Comment