Thursday, August 07, 2014

BAADA YA HOWARD WEBB KUTANGAZA KUSTAAFU, MASHABIKI PINZANI WAENDELEA KUTANIA, CHEKI PICHA WALIZOTENGENEZA!

Shabiki wa United: Mashabiki wengi wa timu pinzani kwa miaka mingi wamekuwa wakimtuhumu Howard Webb kuibeba Man United.

REFA maarufu nchini England, Howard Webb amestaafu kuchezesha soka baada ya kupuliza kipyenga kwa miaka 25. Kocha huyo raia wa England sasa ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa taasisi ya marefa ya (PGMOL).

Webb ni kocha mwenye heshimu kubwa nchini England na amechezesha zaidi ya mechi 500 za ligi kuu na makombe mengine. Pia amechezesha fainali mbili za kombe la dunia, fainali mbili za kombe la Ulaya na ligi ya mabingwa (UEFA). Hata hivyo kwa miaka mingi aliyochezesha mpira, amekuwa akituhumiwa kuibeba Manchester United kwa maamuzi yake.

Hapa chini ni baadhi ya picha za utani zilizopostiwa kwenye mitandao baada ya tangazo la Webb.

Kila la kheri: Manchester City waliposti picha kwenye akaunti yao ya mtandao wa Twita wakimtakia kila la kheri
Webb katika kazi yake mpya

Faida? Howard Webb amekuwa akituhumiwa katika mitandao kuwa kwa muda mrefu amekuwa
akiibeba Manchester United katika mechi zake.

Shangwe: ManchesterUnited wamepata mafaniko makubwa wakati wa uchezeshaji wa Webb

Sir Alex Ferguson alikuwa rafiki wa Marefa wakati akiwa kocha Manchester United

Sanamu: Picha hii inaonesha kuwa Howard Webb amekuwa sehemu ya mafanikio makubwa
aliyoyapata Sir Alex Ferguson katika klabu ya Man United.

Mashabiki pinzani naManchester United wameendelea kutania
baada ya kustaafu wa Howard Webb

Usajili mpya: Usijali, hii ni
picha feki! lakini mashabiki wengi wanaamini Webb alikuwa anaibeba Man United

 BONYEZA HAPA USOME HABARI ZINGINE 

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA ZIPO HAPA

TETESI ZA SOKA ULAYA Atlètico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 25 kuwasajili Javier Hernandez, 26 na Shinji Kagawa, 25, kutoka Manchester United (Guardian), Barcelona wana wasiwasi wa kushindwa mbio za kumsajili Juan Cuadrado, 26, ambaye anasakwa na Manchester United kwa pauni milioni 29 (Daily Star), Liverpool na Tottenham wapo tayari kumfuatilia mshambuliaji kutoka Ivory Coast Wilfried Bony, 25, wakati Swansea wakifikiria kuondoa kifungu cha utenguzi cha pauni milioni 19 cha uhamisho (Daily Mirror), beki wa Arsenal Thomas Vermaelen hatojadili mkataba mpya na Arsenal, katika jitihada zake za kulazimisha uhamisho kwenda Barcelona au Manchester United (Sun), Everton bado wanafikiria kuongeza wachezaji, na wanamfuatilia kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 24 (Daily Mail), Tottenham wanakaribia kukamilisha kumsajili beki wa kati kutoka Argentina, Mateo Musacchio, 23, kutoka Villareal na wapo tayari kumuuza Younes Kaboul, 28, ambaye huenda akahamia Lazio kwa pauni milioni 6 (Telegraph), Pepe Reina huenda akabakia Liverpool baada ya AC Milan kushindwa na mshahara anaotaka (Independent), Sunderland wapo tayari kumfuatilia Samuel Eto'o ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea (Talksport), matumaini ya Liverpool na Manchester United yamezizima baada ya kiungo Marco Reus kusisitiza kuwa atabakia Borussia Dortmund msimu ujao (Metro), Louis van Gaal ataamua wiki hii, nani anabaki na nani anaondoka wakati atakapokamilisha mipango yake ya usajili na Ed Woodward. Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini huenda wakauzwa (Daily Telegraph), Liverpool wanapanda dau la pauni milioni 5 kumtaka beki wa Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo), Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 23.9 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvahlo (O Jogo), beki wa kulia wa Atlètico Madrid Javier Manquillo amewasili Uingereza kufanya vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Liverpool (Daily Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Source salim kikeke

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

Alikiba atoa sababu ya kuunfollow watu wote kwenye Instagram

Baada ya Alikiba kuunfollow watu aliokuwa akiwafollow kwenye akaunti yake ya Instagram ameeleza sababu za kufanya hivyo.

Kupitia mtandao huo, Alikiba ameandika: Thank you for taking time to jot down your opinion . It would be good if you understood my point of view as well . The social platform that keeps me in touch with my fellow artists , fans and others across the world is twitter.

Instagram is limited to pictures… hence more of a preference then an interaction platform . On twitter, I will continue to interact with my fellow artists and celebrities , entertainment and political shareholders , my dear fans and all others See you on twitter and thanks again for taking the time to share your opinion . Much appreciated

Haya ni baadhi ya maoni ya watu wanaomfollow.

Haulefadhili

Inakuwaje hakuna mtu unaye mfollow bro!! Ti me it doesn’t make sense and this means hakuna mtu yyte unaye mpenda au kumkubali or wat?? Wewe kwangu ni kama brother ila kwa hili la (( 0 follow)) silielewi.


Williamkiteleki

Even mi nimekua sana disapointed coz dunia now days imehamia kwenye social netwrk bro kiba..so kwa star kama wewe ukitaka ku coup na mastaa wenzako na hata watu mbalimbali na kujifunza mengine kutoka kwako lazma uwe nao karibu kwenye mitandao ya kijamii(follow them) coz dunian huwezi jua kila kitu kuna vingne lazma utajua kupitia wengne.. dats how life is.. so it will be gud sana kama ukizingatia hili kaka.. unaweza ukaona ni kitu kidgo bt am sure utajifunza vingi kupitia hilo bro

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI ZINGINE ASANTE 

New Music: Nikki Mbishi – Michepuko

Rapper Nikki Mbishi anaye wakilisha Tamaduni Music ameachia ngoma Mpya inaitwa “Michepuko”  BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD 

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE MBALIMBALI 

Shemeji wa Rais Mstaafu Zanzibar ( Mansour Yussuf Himid) Apandishwa Kizimbani na kusomewa mashitaka matatu

Shemeji wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Aman Abedi Karume, Mansour Yussuf Himid, anaendelea kusota rumande baada ya jana kusomewa mashtaka katika Mahakama ya Mkoa wa Vuga kumiliki silaha kinyume na sheria.

Masour alifikishwa mbele ya Hakimu Khamis Ramadhan Abdallah wa mahakama hiyo jana chini ya ulinzi mkali wa polisi na usalama wa taifa na kusomewa mashtaka matatu ambayo yote aliyakana.

Kosa la kwanza kwa mujibu wa muendesha mashataka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Raya Mselem, ni kumiliki silaha aina ya bastola yenye namba F 76172W kinyume na kifungu namba 6 (3) na 34 (1)(2) cha sheria ya silaha na risasi ya mwaka 1991 ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 223.

Mwendesha Mashtaka  huyo  akisaidiwa na Maulid Ali alitaja makosa mengine yanayomkabili Mansoor kuwa ni, kupatikana na risasi 295 kinyume na kifungu  cha 6 (3) na 34 (1) (2) sheria namba 7 ya Zanzibar ya mwaka 1964 na kosa la tatu ni kupatikana na risasi za bunduki aina ya Shotgun 112 kinyume na kifungu cha 34 (1) (2)  sheria ya risasi na silaha  namba 2 ya mwaka 1991.

Baada ya kusomewa mashitaka, Hakimu wa makama hiyo aliamuru mshitakiwa huyo arejeshwe rumande hadi Agosti 18 mwaka huu kutokana na kosa la kwanza kutokuwa na dhamana na makosa mengine kuhitaji kuombewa dhamana.

Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa huyo Omar Said Shaaban aliyekuwa na msaidizi wake Gaspa Nyika, alisema anakusudia kupeleka ombi la dhamana Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Mansor ambaye aliwahi kushika nyazifa mbalimbali katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na CCM kabla ya kuvuliwa uanachama, alikamwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mjini wa Zanzibar.

 HABARI ZINGINE ZIPO HAPA 

Linex nae kaweka nia ya kugombea ubunge,kwa kupitia chama hiki.

Baadhi ya Mastar wa Tanzania wameamua kuweka wazi nia zao za kugombea nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali,miongoni mwa watu hao kwa sasa ni msanii kutoka Kigoma All Stars anaitwa Linex Mjeda.

Amekua wazi kutaja chama ambacho anategemea kugombania nafasi yake ya ubunge aliyosema kuwa tayari ana jimbo anasubiri muda tu na chama alichosema anategemea kugombea ni chama kipya cha ACT.

Soudy Brown amemuuliza maswali mengi ikiwemo kama kweli ana kadi ya chama,sikiliza alichojibu hapa. BONYEZA HAPA KUSIKILIZA 

Source millardayo

Wednesday, August 06, 2014

CHIFU KIUMBE AJIBU MADAI YA KUUZA UNGA...ASEMA SASA AMEAMUA KUMRUDIA MUNGU

Mfanyabiashara maarufu ambaye amekuwa akitoa misaada mikubwa kwa wanamuziki na watu mbalimbali, Chifu Kiumbe amejibu tetesi zilizokuwa zikielezwa na baadhi ya watu kuwa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Chifu Kiumbe amekanusha tetesi hizo katika kipindi cha ‘Mkasi’ na kueleza kuwa yeye hajawahi hata kuyaona madawa ya kulevya.

“Sijawahi kuuza madawa ya kulevya, wala sijawahi kuona unga unafanaje katika maisha yangu. Kwanza katika maisha yangu pombe sijawahi kugusa, sigara sijawahi kugusa wala kinywaji cha aina yoyote.” Amesema Chifu Kiumbe.

Amesema watu wengi katika jamii wana kasumba ya kumsema mtu kuwa anauza unga kwa sababu tu ana pesa nyingi kitu ambacho sio sahihi.

Katika hatua nyingine, Chifu Kiumbe ameeleza kuwa hivi sasa ameamua kumrudia Mungu baada ya kufanya mambo mengi na kwamba anataka kujikita katika kujenga misikiti.

“Nimeamua kurudi kwa mwenyezi Mungu. Nimefanya mengi katika hii dunia na hakuna ambacho sikijui katika hii dunia. Maisha ya kuishi duniani ni machache. Maisha mengi ni kwa mwenyezi Mungu kwa hiyo sasa nimeelekea kwa mwenyezi Mungu na hapa nilipo kiu yangu ni kufikiria jinsi gani ya kujenga misikiti.”

Akizungumzia kitu ambacho anakijutia katika maisha yake, amesema hana anachojutia zaidi ya kuwa na jina kubwa halafu anajikuta akiandikwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa habari zisizo za kweli.

Habari zingine BONYEZA HAPA 

Picha: AY, D’Banj, Fally Ipupa watembelea makao makuu ya benki ya dunia, Washington DC

Fally Ipupa, AY na D’Banj

AY aliongaza na D’Banj, Fally Ipupa na wengine. “Kwanza jana tulikutana na wajumbe wa Youth African Leadership Initiative wale ambao walichaguliwa wakaja hapa kama miezi miwili hivi ambao kwa Tanzania kwa haraka haraka niliwaona ni mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari, Naibu waziri wa Nishati na Madini Steven Masele hao wawili niliwaona na watu wengine wa serIkali ya Zambia pamoja na viongozi mbalimbali wa nnchi za Afrika,”

AY ameiambia Bongo5. “Baada ya kukutana nao hapo sisi tukaenda kwenye rehearsal na introduction na baada ya hapo tukafanya rehearsal pamoja na wasanii wa Afrika ambao walikuja nahisi tulikuwa wasanii tisa au nane kwa sababu hatukuja wasanii wote ambao tulifanya ile project ya wimbo.

Baada ya kumaliza ile function ambayo ilikuwa inafanyika white house watu wakaja kwenye ukumbi ambao ulikuwa unaitwa Newseum ambapo tukafanya kama after party tuka perform. Ilikuwa nzuri sana honestly,” ameongeza AY.

“Kwahiyo tukapiga fresh show nzuri sana, watu walifurahi sana. Tuliperform wimbo mmoja mmoja. Tukaperform mimi na Mwana FA, tukafanya Bila Kukunja Goti, tuliwachezesha mpaka wazee wazee ambao wapo kwenye serikali.

Baada ya hapo tukaperform pamoja wimbo wa Cocoa na Chocolate then baada ya hapo ngoma ikawa imeisha. Leo (jana) hapa najitayarisha tunaenda World Bank na baada ya kwenda world bank halafu tutaenda Capital Center pia tutakuwa na meeting na watu ambao wana uhusiano na white house kwaajili ya kupitisha haya mabilioni kama ambavyo unaona wanayatoa kwenye CNN, Aljazeera na baada ya hapo kunaweza kukawa na after part nyingine I think baadaye kwaajili ya kuangana halafu kesho (leo) kila mtu anaweza kurudi kwake,” amesema.

 HABARI ZINGINE ZIPO HAPA GUSA LINK HII 

Unaikumbuka ile kesi ya Samsung na Iphone?hiki ndicho kilichoamuliwa kwa kampuni hizo.

Ile kesi ambayo inahusu Kampuni ya Apple na Samsung kwa sasa zimekubaliana kuachana na kutupilia mbali kesi zote zilizofunguliwa Marekani zikiwa zimeshitakiana,Kampuni hizo zilizozana kuhusu uanzilishi wa vifaa vya kielektroniki katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Korea ya kusini,Japan na Ujerimani.

Kampuni zote mbili zilikuwa zimewasilisha mashitaka mahakamani lakini katika taarifa yao ya makubaliano ya hivi karibuni,kampuni zote mbili zimesema mzozo huo haukua na jambo lolote linalohusiana na leseni na hivyo basi zitaondoa kesi hizo Marekani.

Mwafaka huu kati ya kampuni hizo mbili umeafikiwa baada ya miaka kadhaa ya migogoro ambapo Migogoro yao ilianza mwaka 2011 baada ya Apple kuishtaki Samsung huko Marekani na kudai kuwa kampuni ya Galaxy iliyoko Kusini mwa Korea ilitumia miundo ya iPhone na iPad.

Kampuni ya Galaxy ilijibu mashtaka ya Apple na kuishtaki kwa misingi ya kuingilia haki zake za uanzilishi wa programu za picha,muziki, na picha za video, na pia jinsi ya kunasa na kutuma picha za video mtandaoni.

Apple pia iliwasilisha mashtaka ya kupinga madai ya uanzilishi na Galaxy lakini hatimaye kuafikiana kutupilia mbali kesi hizo za uanzilishi,Apple ilishinda kesi mbili dhidi ya Samsung miaka michache iliyopita.

Mwezi Mei, mahakama moja ya Marekani iliamuru Samsung kulipa dola million 119.6 kwa Apple kwa kuingilia haki zake za uanzilishi. Apple ilikuwa imewasilisha ombi kulipwa dola milioni 2.2. Vile vile, mahakama hiyo ilikataa kauli kuwa Apple iliingilia haki Fulani za Uanzilishi wa Samsung na kulipa Samsung dola 158,000.

Hata hivyo Samsung ilikana mashtaka hayo na kutaka kulipwa dola milioni 6 kwa madai kuwa Apple ilingilia haki zake za Uanzilishi wa simu Fulani za kisasa zinazoweza kunasa na kupeperusha picha za video Miaka miwili iliyopita, baraza lingine la waamuzi liliamuru Samsung kulipa Apple dola bilioni 1.05 kwa kutumia maarifa ya Apple kutengeneza vifaa vyao, kinyume na sheria.

Habari zipo hapa BONYEZA HAPA 

KUMBE ‘GONJWA’ LA ARTURO VIDAL NDIO SABABU YA LOUIS VAN GAAL KUOGOPA KUMSAJILI

Hatima yake shakani: Bado dili la Man United kuendelea kumsajili Arturo Vidal linaendelea. UHAMISHO wa Arturo Vidal kutoka klabu ya Juventus kwenda Manchester United umeingia shakani kwa sababu nyota huyo wa Chile hayupo fiti, hii ni kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya Chile.

Jorge Sampaoli, alikaririwa huko El Mercurio, akisema bosi wa Man United, Louis Van Gaal anaogopa kutumia paundi milioni 47 kumsajili kwasababu kiungo huyo ana matatizo ya goti.

Vidal kwa muda mrefu amekuwa akiwaniwa na Man United na ripoti zinasema kuwa dili hilo linakaribia kukamilika majira haya ya kiangazi.

Hayupo fiti: Bosi wa Chile, Jorge Sampaoli anasema Louis van Gaal anaogopa kumsajili Vidal kwasababu ya majeruhi. ‘Najua tatizo kubwa katika uhamisho wa Vidali wa dola za kimarekani milioni 80 (paundi milioni 47) kutoka Juventus kwenda Man United, ni Louis van Gaal kuwa na wasiwasi wa kuimarika kwa goti la Vidal,’ Sampaoli aliliambia gazeti la Chile.

Vidal alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi mei mwaka huu na aliharakishwa kupata matibabu ili kucheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
 
BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE