Thursday, August 07, 2014

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA ZIPO HAPA

TETESI ZA SOKA ULAYA Atlètico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 25 kuwasajili Javier Hernandez, 26 na Shinji Kagawa, 25, kutoka Manchester United (Guardian), Barcelona wana wasiwasi wa kushindwa mbio za kumsajili Juan Cuadrado, 26, ambaye anasakwa na Manchester United kwa pauni milioni 29 (Daily Star), Liverpool na Tottenham wapo tayari kumfuatilia mshambuliaji kutoka Ivory Coast Wilfried Bony, 25, wakati Swansea wakifikiria kuondoa kifungu cha utenguzi cha pauni milioni 19 cha uhamisho (Daily Mirror), beki wa Arsenal Thomas Vermaelen hatojadili mkataba mpya na Arsenal, katika jitihada zake za kulazimisha uhamisho kwenda Barcelona au Manchester United (Sun), Everton bado wanafikiria kuongeza wachezaji, na wanamfuatilia kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 24 (Daily Mail), Tottenham wanakaribia kukamilisha kumsajili beki wa kati kutoka Argentina, Mateo Musacchio, 23, kutoka Villareal na wapo tayari kumuuza Younes Kaboul, 28, ambaye huenda akahamia Lazio kwa pauni milioni 6 (Telegraph), Pepe Reina huenda akabakia Liverpool baada ya AC Milan kushindwa na mshahara anaotaka (Independent), Sunderland wapo tayari kumfuatilia Samuel Eto'o ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea (Talksport), matumaini ya Liverpool na Manchester United yamezizima baada ya kiungo Marco Reus kusisitiza kuwa atabakia Borussia Dortmund msimu ujao (Metro), Louis van Gaal ataamua wiki hii, nani anabaki na nani anaondoka wakati atakapokamilisha mipango yake ya usajili na Ed Woodward. Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini huenda wakauzwa (Daily Telegraph), Liverpool wanapanda dau la pauni milioni 5 kumtaka beki wa Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo), Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 23.9 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvahlo (O Jogo), beki wa kulia wa Atlètico Madrid Javier Manquillo amewasili Uingereza kufanya vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Liverpool (Daily Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Source salim kikeke

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

0 comments:

Post a Comment