Tuesday, August 19, 2014

SUAREZ AANZA KAZI RASMI BARCELONA IKIUA 6-0 NA KUTWAA KOMBE

Kungo Xavi akiwa ameshika Kombe la Gamper baada ya ushindi wa 6-0
Ameanza kazi: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez aliyetua kwa Pauni Milioni 75 Barcelona jana ameanza kazi Camp Nou
Lionel Messi akiipangua safu ya ulinzi ya Leon
Lionel Messi akishangilia na Neymar baada ya Mbrazil huyo kufunga

MSHAMBULIAJI Luis Suarez jana ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, Barcelona ikishinda mabao 6-0 Uwanja wa Camp Nou dhidi ya FC Leon, baada ya kupunguziwa adhabu na CAS.

Suarez alifungiwa kujihusisha kabisa na soka kwa miezi minne baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italia kwenye Kombe la Dunia, lakini CAS inapunguza makali yake ya soka kwa kumruhusu kufanya mazoezi na kucheza mechi zisizo za mashindano za Uruguay na Barcelona.

Na jana akaingia kuchukua nafasi ya Rafinha dakika ya 76, wakati huo tayari Barca inaongoza 4-0.

WEMA SEPETU AZIDI KUANDAMWA HUYU NAE AFUNGUKA YA MOYONI AKIMSEMA WEMA AACHE UJINGA!

Mange kimambi ambaye ndiye aliyemuibua Wema Sepetu kwa kumshawishi kushiriki Miss Dar Indian Occean 2006 na hatimaye Wema Sepetu kushinda Miss Tanzania 2006 amefunguka kwa kusema kuwa hawezi kumtetea Wema baada ya Diamond kufunguka kuwa Wema ni mpenda starehe na mashoga wapenda anasa badala ya kujikita kufaya kazi kujiletea amendeleo. Mange amesema kuwa anakubaliana na alichokisema Diamond. Mange ambaye yupo karibu na Wema ameandika . "Mnajua siku zote mimi huwa nakuwa upande wa Wema kwenye issue zake na DIAMOND, Ila leo kwa mara ya kwanza nipo upande wa Shemeji. Wengi wanalaumu kwanini Diamond aweke hiki kitu hadharani ni kama anamdhalilisha Wema. Jamani nimesoma alichoandika huyu kaka what I can say is he really and truely loves Wema ila Wema mwenyewe anaharibu. Yani you can see kabisa he wants the best for his woman ila woman mwenyewe doesn't want the best for herself. Alichosema Diamond ni kwamba yeye kama mwanaume anaweza kumsuport mwanamke wake financially ila kama mwanamke mwenyewe hajisukumi yeye afanyeje sasa?

Alichoandika Maulid Kitenge baada ya kuacha kazi ITV/RadioOne

Home » General News » Alichoandika Maulid Kitenge baada ya kuacha kazi ITV/RadioOne Maulid Kitenge yuko kwenye orodha ya Watangazaji wa muda mrefu wa michezo nchini Tanzania ambapo ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kuanza kufanya kazi na ITV/RadioOne zaidi ya miaka 10 iliyopita. August 18 2014 Maulid aliandika yafuatayo kwenye page yake ya twitter >>> ‘Namshukuru sana Mungu leo nimemaliza miaka 14 ya kutumika kuwa kama mtangazaji wa michezo Radio one stereo na hakika naondoka rasmi‘ Mpaka asubuhi ya August 19 2014 Maulid alikua hajaandika tweet nyingine ya anakokwenda au atakachofanya baada ya kuondoka ITV/RadioOne

MH!! JAMANI MBONA HAKA KATABIA KAMA KANAZIDI KUKUA KWA KASI....

Hebu tuwakanye hawa mabitihivi kesho hawa sindio waanza kudai haki yakuoana?!!!...Tuunganishe nguvu kuwakemea leo..

EXPOSED: HUYU SI JAMAA WA TIP TOP..INAKUWAJE HAPA NA HUYU NYOTA NDOGO WA MOMBASA KENYA!!!!!

BAADA YA UVUMI KUWA LULU AMEMWAGWA NA BEDEJEE WAKE KWAKOSA LA KUCHEPUKA …..NA HIVYO KUNYANNG’ANYWA GARI…..LULU AIBUKA NA KADI ORIGINO YA GARI HILO..SOMA MKASA MZIMA…

Picha Lilianza Hivi Huko Instagram: Baada ya siku za hivi karibuni Lulu Kuposti picha akiwa najamaa ambaye kajifunika kofia ambaye ilisemekana kuwa ndio jamaa anaekula MUZIGO… Chokochoko Leo hiii Toto La Kimanga aliibuka nahii huko instagram; "BbuahahahAaaaa hizi picha zasababisha mdogo wetu kupigwa chin....... Kaa namie nikupe umbeaaa...... Bishost unanijua una kibopa kinachokuweka mujin bila aibu unapost picha na kiserenget bwoy chako unategemea nn??? sasa tutakimbizana na bajaji wallah nahayo ndo madhara yakupewa mkoko without kadi uwiiiiiiiii ukiachwa unanyanganywa kila kitu... haya mereran chali... tmt naye kakupa kibuti poule my toto jamwaaaniii Naskia mshikaji kasharudiana na husna wake sasa sura yako unaiweka wapi mama Wallah sikuile ningekuwa na ndoo ningejaza machoz yako pale kibo complex usikate tamaa kila jambo linasababu yake lol Ulisema tupande milimao eeeh mie yangu na matunda yashaazaa kabisa mixture kutengeneza juise ya limaooooo .......baadae wapendwa" Lulu akajibu..... Akatupia picha ya Kadi ya gari na kuandika;

BALAA GANI HILI MAN UNITED! MAJERUHI WALUNDIKANA MAPEMAA OLD TRAFFORD

Majeruhi: Kiungo wa Manchester United, Jesse Lingard akiondoka kwa msaada wa magongo kutoka hospitali ya Bridgewater, ambako alikwenda kutibiwa mguu wake wa kulia baada ya kuumia juzi katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City Uwanja wa Old Trafford. United ilifungwa 2-1 na beki huyo anaungana na majeruhi wengine wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu, Jonny Evans, Rafael, Luke Shaw, Antonio Valencia, Danny Welbeck, Anderson na Michael Carrick.

Na mdadisiblog/festosaimon

HANS POPPE AFANYA YAKE KIGALI, BEKI LA BURUNDI LAPANDA NDEGE KESHO KWENDA DAR KUJIUNGA NA SIMBA SC

Hakuna kulala; Hans Poppe katikati akiwa na beki wa Telecom, Butoyi Hussein kulia na kushoto ni kipa wa timu hiyo, Jeef Inzokira aliyemsindikiza mwenzake kuzungumza na

Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anampandisha ndege kesho beki wa Telecom ya Djibouti, Butoyi Hussein kwenda Dar es Salaam, baadaye kambini Zanzibar kutazamwa na kocha Patrick Phiri.

Poppe amevutiwa mno na uchezaji wa beki huyo wa kati Mrundi na ameamua kutoa fedha za kumgharimia safari ya Tanzania ili akatazamwe na kocha Phiri- kama akifaa atapewa Mkataba.

Uzuri zaidi, beki huyo amemaliza Mkataba wake na Telecom, hivyo akifanikiwa Simba SC klabu haitahitaji fedha za kumhamisha zaidi ya kupatana na mchezaji mwenyewe pekee.

Poppe aliibuka mjini Kigali, Rwanda mwishoni mwa wiki ambako michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inaendelea na Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amekuwa akihudhuria Uwanja wa Nyamirambo na ndiko alipomuona Butoyi.

Poppe alitua Kigali, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuongeza kwa siku 10 muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Soka Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja.

Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani.

Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.

Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba. Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu. Hata hivyo, Simba SC tayari ina wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, ambao ni mabeki Mganda, Joseph Owino, Mkenya, Donald Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera na Amisi Tambwe pamoja na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera.

Pamoja na hayo, kumekuwa na tetesi kwamba idadi ya wachezaji wa kigeni itaongezwa kutoka watano hadi saba.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

CHELSEA KISIWA CHA MARAHA, YAUA 3-1 DIEGO COSTA AKIHAMISHIA MAKALI YA LA LIGA ENGLAND

CHELSEA imeanza vyema Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 Uwanja wa Turf Moor dhidi ya wenyeji Burnley waliopanda Ligi Kuu msimu huu.

Wachezaji waliompa raha kocha Jose Mourinho usiku huu ni mshambuliaji mpya Diego Costa aliyefunga dakika ya 17, Andre Schrulle dakika ya 21 na Branislav Ivanovic dakika ya 34.

Scott Arfield alitangulia kuwafungia wenyeji mapema dakika ya 14 kabla ya The Blues kugeuza kibao na kuibuka na ushindi huo mnene ugenini, wachezaji wapya wengine Cesc Fabregas, Thibaut Courtois na Didier Drogba wakicheza pia.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Schurrle/Willian dk78, Oscar/Mikel dk82, Hazard/Drogba dk84 na Costa. Burnley: Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Taylor/Kightly dk70, Marney, Jones, Arfield, Ings/Sordell dk82 na Jutkiewicz/ Barnes dk70.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG NASI