Ameanza kazi: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez aliyetua kwa Pauni Milioni 75 Barcelona jana ameanza kazi Camp Nou |
MSHAMBULIAJI Luis Suarez jana ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, Barcelona ikishinda mabao 6-0 Uwanja wa Camp Nou dhidi ya FC Leon, baada ya kupunguziwa adhabu na CAS.
Suarez alifungiwa kujihusisha kabisa na soka kwa miezi minne baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italia kwenye Kombe la Dunia, lakini CAS inapunguza makali yake ya soka kwa kumruhusu kufanya mazoezi na kucheza mechi zisizo za mashindano za Uruguay na Barcelona.
Na jana akaingia kuchukua nafasi ya Rafinha dakika ya 76, wakati huo tayari Barca inaongoza 4-0.
0 comments:
Post a Comment