Tuesday, August 19, 2014

BAADA YA UVUMI KUWA LULU AMEMWAGWA NA BEDEJEE WAKE KWAKOSA LA KUCHEPUKA …..NA HIVYO KUNYANNG’ANYWA GARI…..LULU AIBUKA NA KADI ORIGINO YA GARI HILO..SOMA MKASA MZIMA…

Picha Lilianza Hivi Huko Instagram: Baada ya siku za hivi karibuni Lulu Kuposti picha akiwa najamaa ambaye kajifunika kofia ambaye ilisemekana kuwa ndio jamaa anaekula MUZIGO… Chokochoko Leo hiii Toto La Kimanga aliibuka nahii huko instagram; "BbuahahahAaaaa hizi picha zasababisha mdogo wetu kupigwa chin....... Kaa namie nikupe umbeaaa...... Bishost unanijua una kibopa kinachokuweka mujin bila aibu unapost picha na kiserenget bwoy chako unategemea nn??? sasa tutakimbizana na bajaji wallah nahayo ndo madhara yakupewa mkoko without kadi uwiiiiiiiii ukiachwa unanyanganywa kila kitu... haya mereran chali... tmt naye kakupa kibuti poule my toto jamwaaaniii Naskia mshikaji kasharudiana na husna wake sasa sura yako unaiweka wapi mama Wallah sikuile ningekuwa na ndoo ningejaza machoz yako pale kibo complex usikate tamaa kila jambo linasababu yake lol Ulisema tupande milimao eeeh mie yangu na matunda yashaazaa kabisa mixture kutengeneza juise ya limaooooo .......baadae wapendwa" Lulu akajibu..... Akatupia picha ya Kadi ya gari na kuandika;

BALAA GANI HILI MAN UNITED! MAJERUHI WALUNDIKANA MAPEMAA OLD TRAFFORD

Majeruhi: Kiungo wa Manchester United, Jesse Lingard akiondoka kwa msaada wa magongo kutoka hospitali ya Bridgewater, ambako alikwenda kutibiwa mguu wake wa kulia baada ya kuumia juzi katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City Uwanja wa Old Trafford. United ilifungwa 2-1 na beki huyo anaungana na majeruhi wengine wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu, Jonny Evans, Rafael, Luke Shaw, Antonio Valencia, Danny Welbeck, Anderson na Michael Carrick.

Na mdadisiblog/festosaimon

HANS POPPE AFANYA YAKE KIGALI, BEKI LA BURUNDI LAPANDA NDEGE KESHO KWENDA DAR KUJIUNGA NA SIMBA SC

Hakuna kulala; Hans Poppe katikati akiwa na beki wa Telecom, Butoyi Hussein kulia na kushoto ni kipa wa timu hiyo, Jeef Inzokira aliyemsindikiza mwenzake kuzungumza na

Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anampandisha ndege kesho beki wa Telecom ya Djibouti, Butoyi Hussein kwenda Dar es Salaam, baadaye kambini Zanzibar kutazamwa na kocha Patrick Phiri.

Poppe amevutiwa mno na uchezaji wa beki huyo wa kati Mrundi na ameamua kutoa fedha za kumgharimia safari ya Tanzania ili akatazamwe na kocha Phiri- kama akifaa atapewa Mkataba.

Uzuri zaidi, beki huyo amemaliza Mkataba wake na Telecom, hivyo akifanikiwa Simba SC klabu haitahitaji fedha za kumhamisha zaidi ya kupatana na mchezaji mwenyewe pekee.

Poppe aliibuka mjini Kigali, Rwanda mwishoni mwa wiki ambako michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inaendelea na Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amekuwa akihudhuria Uwanja wa Nyamirambo na ndiko alipomuona Butoyi.

Poppe alitua Kigali, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuongeza kwa siku 10 muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Soka Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja.

Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani.

Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.

Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba. Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu. Hata hivyo, Simba SC tayari ina wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, ambao ni mabeki Mganda, Joseph Owino, Mkenya, Donald Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera na Amisi Tambwe pamoja na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera.

Pamoja na hayo, kumekuwa na tetesi kwamba idadi ya wachezaji wa kigeni itaongezwa kutoka watano hadi saba.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

CHELSEA KISIWA CHA MARAHA, YAUA 3-1 DIEGO COSTA AKIHAMISHIA MAKALI YA LA LIGA ENGLAND

CHELSEA imeanza vyema Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 Uwanja wa Turf Moor dhidi ya wenyeji Burnley waliopanda Ligi Kuu msimu huu.

Wachezaji waliompa raha kocha Jose Mourinho usiku huu ni mshambuliaji mpya Diego Costa aliyefunga dakika ya 17, Andre Schrulle dakika ya 21 na Branislav Ivanovic dakika ya 34.

Scott Arfield alitangulia kuwafungia wenyeji mapema dakika ya 14 kabla ya The Blues kugeuza kibao na kuibuka na ushindi huo mnene ugenini, wachezaji wapya wengine Cesc Fabregas, Thibaut Courtois na Didier Drogba wakicheza pia.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Schurrle/Willian dk78, Oscar/Mikel dk82, Hazard/Drogba dk84 na Costa. Burnley: Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Taylor/Kightly dk70, Marney, Jones, Arfield, Ings/Sordell dk82 na Jutkiewicz/ Barnes dk70.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG NASI 

Monday, August 18, 2014

CHEKI PICHA NNE ZA AMANDA POSHY NI SHEEDAH, KWELI HUYU DADA KAUMBIKA

Maulid Kitenge aacha kazi Radio One/ITV

Mtangazaji mkongwe wa michezo kwenye kituo cha redio cha Radio One Stereo, Maulid Kitenge ameacha kazi.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Kitenge ambaye amefanya kazi kwenye kituo hicho kinachomilikiwa na kampuni ya IPP kwa zaidi ya muongo mmoja, amedai kuwa anakwenda kufanya shughuli zake binafsi akidai kuwa ‘hali ya maisha imepanda kwa kiasi kubwa sana na mahitaji ya kimaisha yameongezeka gharama, hivyo inanilazimu kutafuta njia mbadala ya kujiingizia kipato kikubwa zaidi.’

LULU AWAJIBU WANAOSEMA HAWEZI KUMPATA JUSTIN BIEBER, ASEMA UKICHUKIA UKALE MBEGU ZA MALIMAO

Muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu anaendelea kuonesha hisia zake kwa Justin Bieber na sasa ameeleza kuwa atakuwa anamuandikia ujumbe kila Jumatatu.

Kupitia Instagram, Lulu amepost picha ya JB akiwa kifua wazi akipiga kinanda na kuandika ujumbe akiwajibu wale wanaodai kuwa anaota ndoto za mchana na kwamba hatampata. “ Mapemaaaa...Kabla cku haijawa ngumu..! Haya ni hv wale wa kuandika ndoto za nn cjui...Mara cjui huwezi kumpata na cjui kimepanda kimeshuka...msinijazie comment😂😂😂Acha niwape ufafanuzi kdgo...ni hv Huyu Bwana swala ya yy kupenda....nimemwachia awapende kina @selenagomez na wengine wote anaotaka kuwapenda...ila swala la yy kupendwa Aniachie Mimi....yan hyo kazi yangu....!!! Sasa Kama ni ndoto Wallah ctaki kuamka,Kama ni ufala...yani ninaukubali kwa asilimia 150%,na mengine mengine yote...sasa Kama nakuchefua,Nina uhakika Zile ndimu za @diamondplatnumz haziwezi kukutosha mana hiki kichefuchefu co cha kuisha,bora utafute mbegu ya Malimao au mbilimbi upande kwako kbsa....Na hili Zoezi ni endelevu...yani kila Jumatatu...Kama Mshahara vile....!!! #MCM...... #Nilikuwepo

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

HATA MABONGE NAO HUTOKELEZEA NA MAVAZI YA UFUKWEMNI….!!!!HEBU WACHEKI HAWA!!!

Mara nyingi wanawake wenye mili mikubwa maarufu kama MABONGE NYANYA huwa tuna waweka pembeni kwenye mashwala ya ku- SHOW OFF bikini Body zao ..Eti kuwa hawapendezi.....Sasa watazane hawa harafu niambie kama hawajatokelezea...

NANI AMEKWAMBIA ETI KENYA HAKUNA MA- S3XLY LADIES...!!!! UTACHEKWA...WACHEKI HAPA