Mtangazaji mkongwe wa michezo kwenye kituo cha redio cha Radio One Stereo, Maulid Kitenge ameacha kazi.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Kitenge ambaye amefanya kazi kwenye kituo hicho kinachomilikiwa na kampuni ya IPP kwa zaidi ya muongo mmoja, amedai kuwa anakwenda kufanya shughuli zake binafsi akidai kuwa ‘hali ya maisha imepanda kwa kiasi kubwa sana na mahitaji ya kimaisha yameongezeka gharama, hivyo inanilazimu kutafuta njia mbadala ya kujiingizia kipato kikubwa zaidi.’
0 comments:
Post a Comment