Wednesday, August 13, 2014

Picha: Kampuni ya Japan yatengeneza ‘midoli ya mapenzi’ yenye muonekano halisi wa mwanamke anayevutia!

Kampuni moja ya nchini Japan imedai kufanikiwa kutengeneza midoli ya ngono ‘sex dolls’ yenye muonekano halisi wa mwanamke ambayo huwa na ngozi ya mwili kama ya binadamu na macho kama ya ukweli.

Mdoli wa ngono Orient Industry imesema ni ngumu kuitofautisha midoli hiyo na msichana halisi pale unapoitazama kwa mara ya kwanza.

Midoli hiyo imepewa jina la ‘Dutch Wives’, na matangazo ya midoli hiyo yanasema kuwa iwapo mwanaume akifanya nayo mapenzi hawezi kumtamani mwanamke halisi tena.

Bei ya midoli hiyo ni £1,000 ( zaidi ya shilingi milioni 2.7) kwa kila mmoja. Midoli hiyo imetengenezwa kwa kuweka viungo ambavyo vinamfanya mtumiaji kuigeuza katika position atakayo.
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI           BONYEZA HAPA 

KAVUMBANGU AINUSURU AZAM KULALA KWA WASUDAN

Mkombozi; Didier Kavumbangu ameifungia bao la kusawazisha Azam FC leo Kigali

Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI AZAM FC imepunguzwa kasi katika Kombe la Kagame, baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini jioni hii Uwanja wa Stade de Kigali, Nyamirambo mjini hapa.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Didier Kavumbangu aliinusuru Azam kuzama katika mchezo huo wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 86, baada ya krosi ya Shomary Kapombe.

Azam ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Kipre Michael Balou kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, baada ya pacha wake, Kipre Herman Tchetche kuangushwa.

Atlabara ilirudi vizuri kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 48, mfungaji Nahodha wake, Thomas Batista kabla ya kufunga la pili dakika ya 60 mfungaji Bony Martin.

Atlabara ilipata pigo dakika ya 89 baada ya Nahodha wake, Batista kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Kwa matokeo hayo, Azam inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu na kujihakikishia nafasi ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo, wakati Atlabara inafikisha pointi mbili baada ya mechi mbili.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Gardiel Michael, Shomary Kapombe, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba/Didier Kavumbangu dk63, Leonel Saint Preux na Kipre Tchetche/Khamis Mcha dk63. Atlabara; Jacko Mpenzi, Thomas Batista, Hamza Olema, Hatit Monydeng, Ibrahim Sebit, Kharim Mutawakil, Frando Justin Wani, Joseph Aquer, Dak Kujbor/Khamis Leon dk56 na Bony Martin.
   BONYEZA HAPA KUJINGA NA BLOG HII 

Tuesday, August 12, 2014

BAADA YA DIAMOND SASA NI ZAMU YA CINDY RULZ KUIWAKILISHA VYEMA BONGO KATIKA TUZO HUKO MAREKANI. SOMA HAPA

Baada ya kuepo uvumi wa mda mrefu kua msani Cindy Rulz anatoka kimapenzi na producer Lamar hatimaye Cindy mwenyewe ameamua kufunguka na kusema ukweli wote kuhusiana na ishu hiyo.

Cindy alisema kua Lamar ni kama kaka yake na kamwe hawezi kua na uhusiano nae kimpenzi. Cindy aliyasema hayo jana usiku wakati akihojiwa katika kipindi cha Ala za roho kinachorushwa na Clouds huku mtangazaji akiwa Diva Loveness Love.

Pia Diva alimuuliza kuhusu tetesi za Cindy kuachana mpenzi wake ( Gosby ) na Cindy alisema kuwa hajawahi kuachana na gosby maana kipindi cha nyumba inasemekana alimkuta gosby na wasichana wamemkumbatia wakiwa wanapiga picha so alikasirika akampiga kibao lakini alikiri licha ya kila mahusiano kuwa na matatizo yake.

Wamedumu kwa miaka 6 sasa katika mapenzi yao. Pia Cindy alipata nafasi ya kuwaomba mashabiki wake wote waweze kumpigia kura katika tuzo za Under Ground Music Awards zinazotolewa huko nchini Marekani.

Cindy alisema kua ataenda New York ambako ndipo tuzo hizo zinatolewa kwa ajili ya kuchukua tuzo hizo lakini akasisitiza kua watu anawaomba sana mashabiki wote waweze kumpigia kura.

Jinsi ya kumpigia kura tembelea website hii www.undergroundmusicawards.com na umpigie kura Cindy aliyechaguliwa katika kipengele cha Best African Artist.

Watu wanashauriwa to vote for her ili kumuwezesha kushinda.

 BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI 

DIAMOND UNAHITAJI PONGEZI KWA HIKI ULICHOKIFANYA KWA MSHINDI WA SUPER NYOTA MWANZA

Wakati msako wa kuwatafuta akina dada wanye vipaji vya kuimba kupitia Super Nyota Divas inayoendeshwa na Fetty kupitia Clouds FM ukiendelea katika mikoa mingine 17 baada ya kufanyika katika mkoa wa Mwanza, Diamond aahidi kufanya collable na mshindi wa Super Nyota Akiwa kwenye stage baada ya ku-perform na Lina "Kizaizai" Diamond alitoa tamko hilo akisema

 KAMA BADO UJAJIUNGA NA BLOG HII BONYA HAPA 

NISHER ACHANWA KWA KUSEMA UONGO KUMHUSU PRODUCER HUYU WA VIDEO.

Katika pitapita zangu leo Facebook nkakutana na post ya aliyekua muandaaji mwenza wa Nisher Director wa video za mziki hapa Bongo ikitoa ufafanuzi kuhusu alichokiandika Nisher katika ukurasa wake Facebook. Bamushka amesema kua alichokiandika Nisher ni uongo na huu ndo ukweli aliouandika Facebook

"NISHER WEWE HUKUNIFUNDISHA MIMI NNA ELIMU YANGU KUBWA TU YA PRODUCTION NA ULINIKUTA NAYO....FOR REAL IMESKITISHWA NA POST ZAKO ZOTE MBILI NILIAMUWA KUKAA KIMYA COZ MIMI NI MTU MZIMA NA NAJUWA NINI NAFANYA NA NAJUWA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI UNAISHIA WAPI ... BUT NAONA STIL UNAENDELEA KUDANGANYA WATU KWA KUNICHAFUWA MIMI NIONEKANE NIME KU SNITCH...UKWELI NI KWAMBA SIWEZI FANYA KAZI ISIYO NA FAIDA MIMI NI MTU MZIMA NAHITAJI KU RUN MAISHA YANGU KUPITIA KILE NNACHOKIFANYA ASA KAMA HAKUNA MASLAHI KWANINI NIENDELEE KUWA UNDER YOU? ( sifanyi kazi isiyo na faida ) .... THEN VIDEI ZOTE ULIZO ZITAJA HAPO JUU WEWE HUKUHUSIKA HATA KIDOGO YANI HATA KIDOGO HIZO VIDEO HAZIPO UNDER N.E HIZO ZIPO UNDER ME...MPAKA ZINAFIKA INTERNATIONAL LEVEL U JUST KNOW NOTHING ABOUT IT IS JUT MY OWN POWER...ZINGAITIA HAKUNA ULICHONIFUNDISHA BUT TUMEFUNDISHANA...WEWE HUJANIFUNDISHA WAPO WALIONIFUNDISHA NA WAMEKAA KIMYA... KAMA UMENIFUNDISHA HEBU FANANISHA VIDEO YA CHIN BINZ - LET ME KNOW NA YA LUCCI - SUMU ZOTE NI WHITE SCREEN NA TULITOA AT THE SAME TIME...HIVI NI VIDEO YANGU GANI WE USHAWAHI KUJA LOCATION KAZI YA HIZO ULIZOZITAJA HAPO JUU?... ME SIWEZI LOST A DAYS KUFANYA KAZI ISYONIINGIZIA PESA COZ MIMI SIO KAMA WEWE UKIRUDI HOME UNAKUTA FOOD ON THE TABLE..MEN I DO MY OWN HUSTLING NAHITAJI FIGHT FOR MA OWN...SOO MIMI KUACHA KUFANYA KAZI NA WEWE ISIKUUME KIASI CHA KUKESHA UNA POST POST SHIT ABOUT ME...UKWELI NI KWAMBA NAHITAJI FANYA MISHE ZANGU AU WEWE HUPENDI MIMI NIKIFANIKIWA ? SOMETIMES ETI UNANIKATAZA NISIPIGE STORY NA HIVI WE UNAJUWA ME NA HUYU JAMAA TUMETOKA FAR KIASI GANI ?...MEN ME SIO DIRECTOR WA FACEBOOK WALA INSTAGRAM KAMA WEWE...NYAMAZA LET WORK MAKE NOISE...KUWA MWANAUME SOMETIMES ... AM DONE ... 1 COPPY TO DIRECTOR HANSCANA NA WOTE WANAOTUFAHAMU SINCE DAY 1" Hanscana dE Lavenche Minzi Mims Jozeey Joseph Adam Shani Shine Ande John Cyrill Kamikaze G- The Navigator George Laurent F J Kimbatu Jimmy Cooge Guru G-lover Nisher nae aliandika kua

"Nisher Entertainment Inasikitika kuwataarifu Wadau wake wote na Mashabiki wote wa kazi zetu Kua hatakua Akifanya kazi pamoja nasi Tena! Khalfani Bamushka Ni kama mwaka na Nusu sasa NISHER (C.E.O and President wa NISHER ENTERTAINMENT) Ali-gundua Kipaji Cha khalfani kwa njia ya facebook.. na baada ya hapo walikutana na kuanza kufanya kazi pamoja... Khalfani amejifunza Mengi Kuhusu Video Production Kutoka kwa Mshindi wa Tuzo Za watu 2014 Director Nisher, katika kipindi chote alichokaa kwa karibu sana na Nisher. Khalfani aliweza pia kupata nafasi ya kufanya videos alizozioongoza yeye mwenyewe Chini ya Nisher Entertainment kama "LET ME KNOW" ya iliyo pata kuchezwa Channel O...., pamoja na Video Mpya Ya Baby Madaha, Pamoja na Kazi Nyinginezo Nyingi ambazo zilimwezesha Kupata Jina na Kujiweka vizuri zaidi katika Uongozaji na Uandaaji wa Videos.

Nisher Entertainment Pamoja na C.E.O. wake Tunatambua Juhudi na Bidii aliyokua nayo Khalfani na Tunamshukuru Kwa Mchango wake Katika Kufanikisha Shughuli zote za Nisher Entertainment.

Mwisho....Nisher Entertainment inaendelea kufanya Msako wa Vipaji mbali mbali ili kuwapa Ajira vijana wetu kupitia Mitandao ya kijamii... hivyo wadau wote na wote wale wanao penda kazi zao zionekane Msiache kuzituma kwenye inbox yetu....Tunawashukuru kwa kuendelea ku- Support kazi zetu! Ahsanteni.

NISHER ENTERTAINMENT"

Mganga wa Jadi Aua mgonjwa wake kwa kumtandika fimbo kichwani wakati Akimtibu

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Vicent Kawawa (28) ameuawa kwa kupigwa na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga wa kienyeji aliyekuwa anamtibu ugonjwa wa akili nyumbani kwake katika kijiji cha Buduba kata ya Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Agosti 5 mwaka huu saa 12 jioni.

Alisema Vicent Kawawa(28) mkazi wa kijiji cha Buduba akiwa nyumbani kwa mganga wa jadi aitwaye Mihayo Isheli akitibiwa ugonjwa wa akili aliuawa kwa kupigwa na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga huyo na watu waliokuwepo eneo la tukio na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha tukio hilo ni kwamba mgonjwa alipandisha kichaa na kuanza kumpiga mganga wa jadi na watu waliokuwa eneo hilo na ndipo katika kumtuliza mganga alianza kumpiga akisaidiwa na watu hao ambao idadi yao haijajulikani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema baada ya tukio hilo mganga Mihayo Isheli alikimbia na familia yake pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta mganga huyo na wahusika wengine waliokuwa katika eneo la tukio.

By mdadisiblog/festo saimon

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA HABARI TUPATAPO ZIKUFIKIE KIRAHISI 

Van Gaal awaonyesha Chicharito, Nani mlango wa kutokea Man United

Na festo saimon SIKU chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England na kufungwa kwa pazia la usajili katikia ligi hiyo, Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amewaeleza wachezaji sita akiwamo beki wa kulia Rafael kwamba wanaweza kuchapa mwendo. Marouane Fellaini, Wilfried Zaha, Nani, Shinji Kagawa na kinda yosso Will Keane pia wamevunja 'ndoa' na kikosi hicho cha Van Gaal na hilo limefanyika wakati United ikijifua katika Uwanja wa mazoezi wa Carrington Jumamosi mchana.

Inaeleweka kuwa Mholanzi huyo amewaambia Fellaini, Zaha, Nani na Keane klabu hiyo itasikiliza ofa kwao baada ya kuwaweka sokoni rasmi.

Rafael, alishangaa kusikia jina lake likiwa katika orodha hiyo na kwamba pia anaweza kulazimisha kuondoka wakati huu klabu hiyo ikisaka beki wa kulia.

Kagawa atatumika lakini kaelezwa ataanzia benchi nyuma ya Ander Herrera na Juan Mata. Kiungo Anderson na mshambuliaji Javier Hernandez pia nao tayari wanajua kwamba United itasikiliza ofa endapo zitawasili mezani kwao.

Southampton, Inter Milan, Tottenham, Atletico Madrid na Juventus zote zimeonyesha nia ya kumsajili Mmexico huyo, wakati Napoli itakuwa tayari kumsajili Fellaini kama dili hilo litakubalika na United.

Newcastle inaongoza katika vita ya kumsajili Zaha, huku Crystal Palace, West Ham na Nottingham Forest nazo zikihitaji huduma yake.

Cardiff City imeulizia uwezekano wa kumsajili kwa mkopo Keane ambaye ni pacha wa beki Michael, lakini United inahitaji kumtazama zaidi kabla ya kukamilisha dili hilo.
Kwa sasa United ipo sokoni ikisaka mabeki wapya wawili baada ya kushindwa kumsajili beki wa kati wa Arsenal, Thomas Vermaelen ambaye juzi alijiunga rasmi na Barcelona Mabingwa hao wa zamani wamejipanga kufanya vyema katika msimu huu baada ya msimu uliopita kuboronga na kumaliza kwenye nafasi ya katikati tofauti na mazoea yao.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NA BLOG HII YA MDADISI BONYA HAPA 

KWA HILI WEMA SEPETU UNAISHUSHA HADHI YAKO YA KUWA MKE WA DIAMOND PLATNUMZ

Mara nyingi Wema amekuwa akimsupport mchumba wake kwa kupanda naye jukwaani na hivyo kusababisha shangwe kubwa.

ushabiki wa Wema kwa Diamond kidogo umepitiliza na hata kama umekuwa ukishangiliwa, tunahisi anajishusha kiaina.

Kuna ile hadhi ya mke lazima ilindwe hasa kama mke ama mpenzi wako si msanii kama wewe.

Wema ni muigizaji si dancer ama mwanamuziki na kwa muigizaji wa filamu mwenye mashabiki wengi, kupanda jukwaani na kukata viuno design kama ni kushusha brand ama nini? Si mbaya kama angekuwa akipanda na kutoa salamu fupi kisha kushuka na kuwa mtazamaji kama watu wengine. Tupe Mtazamo wako
 BONYEZA HAPA 

HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA LADY JAYDEE, YADAIWA NDOA YAKE NA GARDNER YAVUNJIKA.

Ndoa ya mwanuziki Jay dee na mtangazaji mashuhuri wa radio Gardner G. Habash inasemekana imevunjika huku Gardner akihama Kimara alikokua akiishi na mkewe na kuhamia kwa moja wa ndugu zake wa karibu sana.

chanzo cha kuvunjika ndoa hiyo bado hakijajulikana moja moja kwa moja ila wawili hao wamekuwa katika migogoro kwa muda.. na si mara ya kwanza kutengana ila this time hali si shwari. yazidi kusemekana kaka Gardner kazidi michepuko amekua haibi tena anafanya bayana mpaka mwenye mali anajua anavyoibiwa.

kudhihirisha hayo katika ukurasa wake wa IG dada jide ameandika "Walking Away From Troubles" ambapo umbepuzi yakinifu waonesha mambo si sawa hata kidogo. Gardner kabla ya kumuoa Jide alikua tayari na mke halali wa ndoa na mtoto mmoja.

 BONYEZA HAPA KAMA BADO UJAJIUNGA NASI  

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMANNE ZIPO HAPA

Beki wa Liverpool Kolo Toure, 33, anajiandaa kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki katika mkataba wa pauni milioni 1.5 (Daily Mail), boss wa Liverpool Brendan Rodgers anafikiria kumchukua mshambuliaji kutoka Cameroon, Samuel Eto'o, 33, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea msimu uliopita (Guardian), Galatasaray wanafikiria kutoa pauni milioni 28 kuwachukua Joel Campbell, 22, na Lukas Podolski, 29, kutoka Arsenal (Daily Express), QPR wapo tayari kumtoa Loic Remy, 27, kubadilishana na Andros Townsend, 23, na Harry Kane, 21 kutoka Tottenham (CaughtOffside), Remy pia huenda akawindwa na Chelsea, wakati Jose Mourinho akitafuta mchezaji wa kuziba pengo la Didier Drogba, 36, aliyeumia (Goal), kiungo kutoka Spain Santi Cazorla, 29, ametupilia mbali tetesi kuwa anataka kuondoka Arsenal na kurejea La Liga (Daily Mirror), Stoke City wamepanda dau jipya na kutoa pauni milioni 5 kutaka kumchukua winga wa Norwich Nathan Redmond, 20 (Daily Mail), Aston Villa wanakaribia kumchukua Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 3.5 (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba huenda asiweze kucheza kwa miezi minne baada ya kuumia 'enka' katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ferencvaros (Daily Mirror), Southampton huenda wakampiga faini Morgan Schneiderlin, 24, iwapo kiungo huyo Mfaransa atakataa kucheza mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili (Daily Telegraph), kipa wa Manchester City Willy Caballero, 32 amemwambia kipa mwenzake Joe Hart, 27, atalazimika kupigania namba moja, Etihad (Telegraph), Chelsea wanamfuatilia beki wa kati wa Roma, Mehdi Benatia, 27, ambaye anadhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30 (Daily Mirror), Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 10 kumshawishi beki wa kati wa Liverpool Daniel Agger (The Sun), Everton na Tottenham wako 'macho' baada ya kuambiwa Salomon Kalou anaweza kuondoka Lille kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Daily Mirror), Arsenal wapo tayari kumfuatilia beki wa Olympiakos Kostas Manolas kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Daily Express).

 KAMA BADO UJAUNGANA NASI BONYEZA HAPA