 |
| Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye
vituko ambae alipata umaarufu sana toka
akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake
kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae
anaingia na hereni bungeni, blingbling
kibao kama cheni na pete kama
anavyoonekana ametupia kwenye hii picha
hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la
Nairobi.Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta
alikwenda The Hague Uholanzi kwenye
Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya
wenzake wanaopinga huo uamuzi wa ICC
na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli
zao ili kwenda kumsupport ambapo Seneta
huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia
wengine pia.
Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na
dukuduku la kukerwa na maamuzi ya
Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao
wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa
tshirt yenye maandishi ya Kiswahili
‘ikiwatusi’ Wazungu kama anavyoonekana
kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana
Seneta wa jiji la Nairobi Mike Sonko akiwa
amewasili mahakamani ICC na kikosi
chake kisha wakafanya maandamano
mafupi kabla ya kumpa support Rais
Uhuru kwa kuimba wimbo wa taifa na
nyimbo za kizalendo wakati kesi ya Uhuru
ikiwa inaendelea Mahakani. |
 |
| Tayari Rais Uhuru Kenyatta amerejea
Kenya jana asubuhi na kupokewa na
maelfu ya Wakenya ambao
hawakupendezwa na kilichofanywa na
Mahakama hiyo. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment