| Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Uganda, Milutin Sredojevic
‘Micho’ amemuengua kikosini mwake
mshambuliji Mganda, Emmanuel Okwi baada
ya kuonyesha kiwango cha chini akiichezea
The Cranes dhidi ya Togo Jumamosi.
Uganda inaondoka jioni ya leo kwenda Togo
kwa ajili ya mchezo wa marudiano Kundi E
Kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika huko
Okwi akirudishwa Dar es Salaam
akaimarishe kiwango kwenye klabu yake
Simba SC.
“Ndiyo, nimelazimika kufanya hivyo
(kumuacha Okwi),”amesema Micho
akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni ya leo
kwa simu kutoka Kampala, Uganda.
Micho pia amemuacha Nahodha wake, Andy
Mwesigwa, ambaye anatumikia adhabu
baada ya beki huyo wa FC Ordabasy ya
Kazakhstan kufikisha kadi mbili za njano
ikiwemo ya jana, Uganda ikilala 1-0 Uwanja
wa Namboole.
Kikosi cha Uganda kinachoondoka leo ni,
makipa; Robert Odongkara na Dennis
Onyango, mabeki; Dennis Guma, Godfrey
Walusimbi, Savio Kabugo, Isaac Isinde,
Martin Kizza na Murushid Jjuuko, viungo ni:
Tonny Mawejje, Aucho Khalid, Geoffrey
'Baba' Kizito, Brian Majweja, Kizito Luwagga
na Moses Oloya, wakati washambuliaji ni
Geofrey Massa (Nahodha), Daniel
Sserunkuma, Yunus Sentamu na Brian
Umony.
Baada ya kutemwa na Uganda, Okwi sasa
atalazimika kuwahi kambi yake ya klabu
yake, Simba SC nchini Afrika Kusini ambayo
imejificha kujiandaa na mchezo dhidi ya
watani, Yanga SC Oktoba 18, Dar es
Salaam.
Okwi anaweza kuondoka pamoja na
wachezaji wa Simba SC walio katika timu ya
taifa, Taifa Stars mabeki Miraji Adam na
Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude,
Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna
Chanongo. Stars inacheza na Benin jioni hii
Dar es Salaam na wachezaji hao
wanatarajiwa kuondoka kesho. |
0 comments:
Post a Comment