| Katika hali isiyokuwa ya kawaida , mpigadebe
maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi
wilayani mbeya amenunua mbuzi wawili na
bidhaa nyingine za aina mbalimbali zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na
kuzipeleka kwenye vituo vya watoto yatima
kama zawadi huku akiwaasa watoto hao
kutoshawishika kwenda kupiga debe kwenye
vituo vya mabasi.
Mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha
mbalizi, Anganile Mwamuluma Andrea ambaye
amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20
ameushangaza umma wa wakazi wa mbeya
baada ya kuamua kununua mbuzi wawili,
mchele , maharagwe, sabuni, mafuta ya kupikia
na mahindi na kupeleka bidhaa hizo katika vituo
viwili vya watoto yatima ambako amezitoa kama
zawadi kwa watoto hao , huku akiwaasa
kutoshawishika kujihusisha na kazi ya kupiga
Debe kwenye vituo vya mabasi . |
0 comments:
Post a Comment