| Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi
amefukuzwa kazi na shirikisho la soka nchini
humo, NFF mapema Alhamis hii licha ya timu
yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya
Sudan jana.
Keshi ametimuliwa pamoja na makocha wake
wasaidizi Daniel Amokachi na Ike Shorunmu. NFF
imemshukuru Keshi na wasaidizi wake kwa kazi
waliyoifanya na imeahidi kuwalipa mafao yao
ndani ya wiki mbili zijazo.
NFF, imedai kuwa Keshi, Amokachi na Shorounmu
wanaweza kuendelea kusoma course yoyote ya
ukocha katika nchi wanayotaka ili kuboresha
uwezo wao. |
0 comments:
Post a Comment