Saturday, October 04, 2014

MESS MATATANI KWA KUKWEPA KODI

Nyota wa timu ya Barcelona na Argentina Lionel
Messi anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji wa
kodi,hii ni kwa mujibu wa jaji mmoja wa
Uhispania.
Jaji huyo amepinga ombi la kiongozi wa
mashtaka la kufutilia mbali mashtaka hayo kwa
madai kwamba babake mchezaji huyo ndiye
anayesimamia fedha zake.
Messi na babaake Jorge wanashtakiwa kwa
kuiibia mamlaka ya taifa hilo zaidi ya yuro
millioni 4.
Wote wamekana kufanya makosa hayo yalioanza
mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment