Saturday, October 04, 2014

HII NI HABARI MPYA NA MBAYA KWA TAMBWE NA OKWI

HABARI mbaya kwa Emmanuel Okwi na Amissi Tambwe ni kwamba yule beki mbishi wa Stand United, Yassini Mustapha “Evra” amerejea na atakuwepo kwenye mchezo wao na Simba leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa. Mwenyewe ametamka wazi kuwa mastraika hao wajue fika wana kazi kubwa naye, beki huyo wa kushoto hakucheza mechi mbili za mwanzo kutokana na kuchelewa kwa leseni yake baada ya klabu aliyokuwa akiichezea ya Polisi Dodoma kumwekea pingamizi lakini sasa mambo yamekwisha. Akizungumza na Mwanaspoti, beki huyo alisema kulikuwa na matatizo na klabu yake ya zamani ya Polisi Dodoma jambo lililofanya ashindwe kucheza mechi mbili ya Ndanda FC na Mgambo JKT ambapo leseni yake ilikuwa haijatoka lakini sasa mambo yako safi. “Sijawahi kucheza nao hawa washambuliaji wa Simba huyo Okwi na Tambwe ila nataka kusema wana kazi kubwa na mimi hilo wajiandae kabisa hakuna wa kupita kwangu,”alisema huku kocha msaidizi wa klabu hiyo Athumani Bilali akithibitisha atacheza.

CREDIT MWANASPOTI

0 comments:

Post a Comment