Saturday, October 04, 2014
|
Wakati mkataba wake wa mkopo ukiwa
umebakisha miezi nane kuisha, usajili wa
Radamel Falcao kwenda Manchester United
umechukua nafasi kwenye vyombo vya habari
vya Uingereza vinavyoripoti kwamba Man
United imekubaliana rasmi na mahitaji binafsi
ya mchezaji huyo kwa ajili ya kukamilisha
usajili wa kudumu.
Taarifa zinaeleza kwamba Man United
wanafanya jitihada zote kumaliza suala la
usajili wa Falcao ili kuepuka kila kilichotokea
miaka mitano iliyopita katika usajili wa Carlos
Tevez……. United walimsajili Falcao kwa mkopo
kutoka Monaco siku ya mwisho ya usajili wa
wakati wa kiangazi.
Wakiwa tayari wameshalipa ada ya mkopo wa
£6million kwa klabu ya Ufaransa, United pia
walishakubaliana kimsingi na Monaco kuwalipa
kiasi cha £43.5m ikiwa wataamua kumchukua
Falcao kiujumla mwishoni mwa msimu.
Baada ya hayo yote, leo imeripotiwa kwamba
mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward
tayari amekubaliana na wawakilishi wa Falcao
kumlipa mshahara wa £250,000 kwa wiki
mchezaji huyo pamoja na bonasi na haki za
taswira yake kutumika ambapo kwenye
sentensi nyingine club hii imekanusha taarifa
kwamba itakatisha mkataba wa mkopo wa
Falcao ikiwa mchezaji huyo ataumia tena goti. |
Na mdadisiblog
0 comments:
Post a Comment