Wednesday, October 15, 2014
 |
| Hivi karibu msanii mahiri na nguli katika tasnia
ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu
kama Lulu ataibuka na filamu yake Mpya na
yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU"
ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo
ni Bi Flora Mtegoha ambaye ni Mama Mzazi wa
aliyekuwa msanii nguli wa kiume hapa 'Bongo'
marehemu Steven Kanumba.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya
filamu ambayo Lulu ameonesha uwezo wa hali
ya juu na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya
wasanii wa kike hapa Tanzania ambaye
ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika
ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika
kutokana na muongozo anaopewa.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa sokoni
hivi karibuni kwa wauzaji wa filamu kote nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya
Proin Promotions Ltd. |
0 comments:
Post a Comment