| Kesi ya utekaji iliyokuwa ikimkabili Madee
imemalizika kwa kulipa faini ya shilingi
50,000. Madee alidaiwa kumteka kijana
mmoja huko Kigamboni baada ya kumuibia
simu. Hakimu ametoa hukumu ya kifungo
cha jela miezi sita au kulipa faini ya kiasi
hicho cha fedha. Madee alilipa faini.
Madee amezungumza kwa mara ya kwanza
tangu apatwe na mkasa huo.
“Yule dogo baada ya kuniibia simu
tulimgonga kwa nyuma akaanguka
tukamwokota na kumbeba kwenye Noah
yetu tukaondoka naye. Kesho yake
nilikuwa na safari ya kwenda Mwanza
kwahiyo nikaachia masela wampeleke
polisi na hapo mimi nilishampigia simu
mama yake ili aongee na mwanae aseme
simu yangu iko wapi. Simu yangu yenyewe
ndio ilikuwa kila kitu. Kwahiyo
nilivyoondoka nikiwa sina hata
mawasiliano, nikaenda Mwanza nimefanya
show, nimerudi Jumatatu asubuhi
nikaulizia mtuhumiwa wangu nikaambiwa
yupo Magomeni. Nikaenda Magomeni polisi
nikaambiwa dogo kahamishiwa
Kigamboni,” amesimulia Madee.
“Nikaamua kwenda Kigamboni, kwenda
Kigamboni nikaambiwa ‘bwana wewe ndo
unashtakiwa ukitaka kumteka huyu dogo’
ndio nikawekwa ndani, nikalala siku moja,
asubuhi nikadhaminiwa nikatoka kesi
ikaenda mahakamani. Mahakamani kesi
ikaahirishwa siku ya kwanza siku ya pili
ikapita, hukumu nikaambiwa kati ya
kwenda jela miezi sita au kulipa faini
50,000. Nikalipa faini na kesi ikaisha.
Yaani mimi ndo nimekuwa mwenye kosa,
mimi ndo niliyelipa faini.” |
0 comments:
Post a Comment