East Africa Television (EATV)
MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU ANA
MIAKA 23 NA SIO 18
Katibu wa kamati ya Miss Tanzania Bosco
Majaliwa amesema kuwa mshindi wa Miss
Tanzania 2014 Sitti Mtemvu amezaliwa mei 31
mwaka 1991 na umri wake sahihi ni miaka 23 na
sio miaka 18 kama ilivyozagaa sehemu
mbalimbali.
Katibu huyo aliongeza kuwa Sitti ana shahada
ya ya uhusiano wa kimataifa na alimaliza
masomo yake Desemba mwaka jana katika chuo
kikuu cha North Texas kilichoko kwenye jiji la
Dallas nchini Marekani.
Sitti Mtemvu bado hajasoma ngazi ya shahada
ya uzamili (Masters) kwa sasa ila anatarajiwa
kwenda kusoma ngazi hiyo huko nchini
Marekani. |
0 comments:
Post a Comment