Stori: Andrew Carlos
BAADA ya kuandamwa na skendo kuwa anatoka
kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul
‘Diamond’, mkali wa Bongo Fleva, Meninah
Abdulkareem ‘Meninah la Divah’ amesema yuko
mbioni kumtambulisha mchumba wake.
Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’.
Akipiga stori na gazeti hili, Meninah ambaye ni
zao kutoka shindano la kuibua vipaji vya kuimba,
Bongo Star Search ‘BSS’ 2012 alisema;
“Nimechoshwa kila siku kusikia Diamond, sasa ni
bora nimtafute mwanaume yeyote tu kisha
nimtambulishe ili ijulikane siko na Diamond,”
alisema Meninah ambaye yupo mbioni kuachia
ngoma mpya ya Kaniganda.
Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’
akipozi.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Meninah
anatoka kimapenzi na Diamond, pia Diamond
ameshafika kwao kujaribu kutoa mahari ili
amuoe.
0 comments:
Post a Comment