Thursday, October 16, 2014
 |
| Kama ulikuwa unawasiwasi kuwa haitawahi
kutokea collabo ya Diamond na msanii mwenzake
ambaye alikuwa akitajwa kuwa na tofauti nae
Alikiba, sasa unaweza kupunguza mashaka
sababu Diamond yupo tayari kuingia booth na
mwimbaji huyo wa ‘Mwana’ endapo atatakiwa
kufanya hivyo (lakini endapo kama na Alikiba
atakuwa tayari kwa ofa hiyo).
Diamond Platnumz amesema yupo tayari kufanya
collabo na Alikiba au msanii yeyote atakayehitaji
msaada wake.
“Mimi sina tatizo, inategemea ni project gani
inategemea ni muziki gani kwasababu
nimeshawasaidia watu wengi nimefanya nao
macollabo kwanini mtu anavyokuja nifanye nae
collabo yeye nikatae, yaani siwezi kukataa”
Diamond ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“mwaka huu kwanza zitatoka nyimbo nyingi za
macollabo ambayo wasanii wengi wa Nigeria
nimewasaidia nimefanya nao nyimbo, wengi sana.
Kcee nimefanya nae, nimefanya na Mafikizolo,
nimefanya na yule Waje, nimefanya na Don Jazzy,
nimefanya na Dr Sid, nimesaidia watu wengi
sana. Kwahiyo kama naweza kufanya wa huko
kwanini nisifanye na mtu wa nyumbani,
nikishindwa kufanya na mtu wa nyumbani
nitakuwa na roho mbaya, au nitakuwa sitaki
kusaidia kwasababu namshukuru mwenyezi
Mungu muziki wangu kidogo umefika hatua sio
mbaya, so nikifanya na mtu wa nyumbani na yeye
namfikisha katika hatua ambayo hajawahi kufika
bado, so mi siwezi kumkatalia mtu yeyote”.
Ni hivi karibuni tu msanii Wizkid wa Nigeria nae
alipoulizwa swali kama hilo kama ikitokea
akatakiwa kufanya collabo na mpinzani wake
Davido, nae alisema kila kitu kinawezekana. |
0 comments:
Post a Comment