Tuesday, October 14, 2014
 |
| Diamond na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva
wenye timu mbili kubwa za mashabiki
waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba
yao, Team Diamond v/s Team Alikiba, ushindani
ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo
Nasib Abdul amedai kuwa haipo.
Platnumz ambaye alikuwa bado hajaamua
kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka juu
ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa
inazungumzwa baina yake na muimbaji huyo wa
‘Mwana’.
“Nimekua nikiskia muda mrefu vimezungumziwa
sana, kwenye mitandao katika nini, sijui kwanini
vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya
Clouds Fm “Unajua kuna time ikifika inabidi
uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu
havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa
unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye
atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa
nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu,
atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe
mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi
kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.
“Tangia mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga
hivyo ilikua sijui kwa Belle 9, ilitoka kwa Belle 9
ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja sijui
kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali
tena ikaja ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean
Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa Richard
Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda
unafanya vizuri hivyo vitu vinakua vinatokea, so
ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa
na upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana
tatizo kumbe si tatizo ni vitu ambavyo vitakuwepo
tu kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu
anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika
kazi inayofanana hivyo vitu vitatokea yaani watu
watashindanisha, unaweza hata ukashindanishwa
na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.
“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna
kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa
Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye
mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini
haimaanishi Simba na Yanga ni maadui
wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah
ah..”
Diamond amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na
tatizo na yeye anaamini angeweza kumfata na
kumwambia sababu amefahamiana nae kabla
hajakuwa mwanamuziki.
“Sasa hivi yaani karibia mwaka wa tano, Mi
tangia nianze kufanya muziki sijawahi kudrop kila
siku nazidi kupanda juu…so hivyo vitu lazima
vitatokea lazima nivikubali, inawezekana we
unasema we unasema we hauna tatizo lakini
mwenzio akawa anahisi wewe una tatizo nae,
lakini naamini kama angekuwa anahisi kama
mimi nina matatizo na yeye angenifata
akaniambia kwa sababu mimi sijajuana na Ali
kwenye muziki, nimejuana na Ali kabla sijakuwa
mwanamuziki, nimemjua Ali kupitia dada yangu
Queen Darleen so alikuwa an uwezo wa kunifata
akaniambia personally kwamba bana umefanya
hichi na hichi na hichi”.
Diamond amemaliza kwa kusema kuwaomba
media na mashabiki wasifanye ionekane kama
wana beef binafsi bali wazishindanishe kazi ili
kukuza muziki wa Tanzania.
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama
kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni
vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya
kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana
media na watu wasitengeneze kufanya kama ni
matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa
inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi
na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya
watu wawe na changamoto ya kusema ngoja
nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha
muziki wetu ukue.” |
0 comments:
Post a Comment