Saturday, September 27, 2014
 |
MPANGO wowote wa kuongeza muda wa
Frank Lampard kuendelea kucheza kwa
mkopo Manchester City unaweza kuibua
maswali zaidi ya kimaadili juu ya uhamisho
wake, kwa mujibu wa kocha Arsenal, Arsene
Wenger.
Lampard alisaini timu ya Ligi Kuu ya
Marekani (MLS), New York City baada ya
kutemwa Chelsea, kabla ya kurejea ghafla
Ligi Kuu ya England kujiunga na mabingwa,
ambao pamoja na kuinunua timu ya
baseball ya nchini humo, wakanunua na
hisa timu hiyo ya MLS.
Kiwango kizuri cha mkongwe huyo mwenye
umri wa miaka 36, aliyefunga mabao mawili
katika ushindi wa 7-0 Kombe la Ligi,
maarufu kama Capital One Cup dhidi ya
Sheffield Jumatano, kimeibua tetesi kwamba
City itaangalia uwezekano wa kumbakiza
ifikapo Januari.
Frank Lampard alijiunga na Man City kwa
mkopo wa muda mfupi baada ya kuondoka
Chelsea msimu huu
Msimu wa MLS 2015 unatarajiwa kuanza
tena Machi, mwakani na Lampard amesema
hajafanya majadiliano yoyote na City juu ya
mustakabali wake mwishoni mwa mwaka.
Wenger, ambaye alimrudisha kwa mkopo
Nahodha wake wa zamani The Gunners,
Thierry Henry kutoka New York Red Bulls
Januari 2012, anaamini namna yoyote ya
kuongeza mkataba wa mkopo wa Lampard
kwa sasa haitakuwa nzuri, hata ikiwa ni
ndani ya utaratibu wa Ligi Kuu.
"Wakati wote una maamuzi ya aina mbili,
moja ya kimaadili na pili ni ya kisheria na ni
juu ya unavyochukulia,"amesema Wenger.
"Nafikiri, hii ni sheria? lazima uheshimu hilo
na kisha mchezaji lazima atazame uamuzi
wake. Naheshimu ukweli kwamba anataka
kucheza katika kiwango cha juu na labda
hakuwa na nafasi zaidi Chelsea. Sijui haswa
kilicho nyuma ya hili,".
"Ulikuwa ni mpango wake kwenda New York
na kwenda Man City? Sina uhakika. Nafikiri
kabisa alitaka kwenda nje na kutua New
York, na (kisha) kupewa ofa ya kurudi Ligi
Kuu England na kuichukua. Anaweza
kufafanua vizuri yeye mwenyewe kuliko
ninavyofanya, sijui nini kipo nyuma ya
hili,"amesema Wenger. |
0 comments:
Post a Comment