Tuesday, September 16, 2014

UNYAMA WA KUTISHA DAR: ACHINJWA NA KUTUPWA, AOKOTWA NA WATOTOT WAKE WADOGO!

Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa. Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike katika eneo hilo mwaka 2005. Akizungumza kwa uchungu na Uwazi, mke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani), alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti. Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora walielekezwa kwa marehemu huyo. Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu.

Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment