Monday, September 22, 2014
|
Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu
wa Simba, Abdallah
Kibadeni, amesema
mshambuliaji wa kimataifa
wa Simba, raia wa Uganda,
Emmanuel Okwi, anateswa na
mzimu wa marehemu, Patrick
Mafisango kwa kuwa ndiye
aliyekuwa akimchezesha.
Okwi amesajiliwa na Simba
katika dakika za mwisho
lakini alikuwa hajaonyesha
ubora wake kwenye mechi za
kirafiki alizocheza kabla
ya jana kuivaa Coastal.
Kibadeni amesema Okwi
anahitaji ajipange ipasavyo
ili aweze kupata nafasi ya
kucheza Simba na kumpata
mtu wa kumchezesha kama
ilivyokuwa kwa Mafisango
ambaye ndiye aliyekuwa
msaada mkubwa kwake.
“Okwi ninayemjua mimi si
huyu wa sasa kwani kiwango
chake kimeshuka mno, hivyo
anahitaji kujipanga
ipasavyo kwa kuonyesha
juhudi za hali ya juu ili
aweze kupata nafasi katika
kikosi cha kwanza.
“Zamani wakati anaichezea
timu hiyo alikuwa na mtu wa
kumchezesha, marehemu
Mafisango, hivyo kwa sasa
anahitaji mtu mwingine
aweze kumchezesha na kuwa
katika kiwango kizuri kama
cha awali,” alisema
Kibadeni. |
Posted via Blogaway
pamoja sana hii
ReplyDelete