Saturday, September 20, 2014
 |
| Msanii wa filamu Bongo , Kajala Masanja
akiwa na mumewe mahakamani .
Licha ya mkwanja kumtembelea , msanii wa
filamu Bongo , Kajala Masanja amekwama
kupata pesa ya kumlipia faini mumewe
Faraji Chambo ili aweze kutoka
jela .Akizungumzia ombi la mumewe huyo
kumtaka kutofuja pesa badala yake amlipie
faini ili aondokane na mateso ya gerezani,
Kajala alisema ni kweli anampenda sana
mumewe na angetamani kufanya hivyo
lakini kiasi cha shilingi milioni 200
kinachotakiwa si kidogo hivyo hawezi
kukipata.
“ Nampenda sana mume wangu , hilo halina
ubishi na pia najua anateseka sana kule
gerezani kwani nakujua lakini milioni 200
siyo hela ndogo ujue . “ Natamani hata leo
niwe nayo nimlipie lakini ndiyo hivyo tena ,”
alisema Kajala kwa masikitiko .
Hata hivyo , licha ya Kajala kuwa na nia ya
kumtoa jela mumewe , mmoja wa mawakili
aliyekuwa akihusika na kesi yao aliyeomba
hifadhi ya jina lake alisema:
“ Kama Kajala anafikiria kumlipia mumewe
faini simshauri afanye hivyo kwani hukumu
iliyotolewa ni ya kesi moja na ile nyingine
ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa
bondi na Takukuru , bado inaendelea na
huwa Faraji anatoka gerezani kwenda
mahakamani.
“ Sasa Kajala anaweza kutoa pesa zake ,
mumewe akatoka lakini hukumu ya ile kesi
nyingine ikatolewa na akarudi tena jela ,”
alisema wakili huyo. Hivi karibuni, mume
wa Kajala alituma ujumbe kupitia watu
wanaokwenda kumtembelea akimtaka
mkewe kumuonea huruma na kumlipia faini
ili atoke gerezani badala ya kuzitumia pesa
kwa anasa. |
0 comments:
Post a Comment