Friday, September 26, 2014

Hospitali imesemaje kuhusu mchezaji wa Uganda aliefariki baada ya goli la Lampard?

Marehemu ni huyu alievaa jezi ya njano
Kabla ya kifo chake Musana alifanya mazoezi na timu yake Jumapili asubuhi na kula chakula cha mchanana mmoja wa marafiki aitwae Gerald Bagoole na kisha wakati wa mpira alikwenda kutazama jirani na anapoishi.Habari za kuhuzunisha za mashabiki wa soka Uganda zimekua na mfululizo wake kwenye hii miaka miwili huku wengine wakijiua baada ya kushindwa mechi na mmoja akiwana majonzi ya nyumba yake baada yakuiweka rehani akishadadia kutabiri ushindi wa timu yake.

Ni taarifa ambayo ilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba mchezaji wa club ya Simba ya Uganda Fahad Musana amefariki kutokana na mshtuko wa goli alilolifunga Frank Lampard wa Manchester City wakati wakicheza naChelsea juzi.

Pamoja na hayo, taarifa kutoka hospitali kuu Uganda ya Mulago zinasema Fahad alifariki kutokana na ugonjwa wapnemoniana sio mshtuko uliotangazwa awali ambapoFahad aliezikwa September 24 2014 baada ya kufia kwenye hospitali ya Bombo Barracks alikua shabiki mkubwa wa Chelsea.

0 comments:

Post a Comment