Saturday, September 20, 2014
 |
| BEKI wa pembeni wa Arsenal, Mfaransa
Mathieu Debuchy anaweza kuwa nje ya
Uwanja hadi Krisimasi baada ya kuumia
enka dhidi ya Manchester City mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Kocha Arsene Wenger amesema kwamba
Debuchy alitarajiwa kwenda kufanyiwa
uchunguzi kama atahitaji upausaji wa
kifundo chake cha mguu jana jioni ambao
utatoa majibu atakaa nje kwa muda gani.
Ikiwa hatahitaji upasuaji, itamchukua wiki
sita nje ya Uwanja kabla ya kurejea dimbani,
lakini kama atapigwa 'kisu' atakuwa nje
kwa angalau miezi mitatu. |
0 comments:
Post a Comment