Thursday, September 25, 2014
 |
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIPA namba moja wa Simba SC, Ivo Philip Mapunda amevunjika kidole mazoezini Zanzibar leo asubuhi na anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane- maana yake hataweza kusimama langoni timu hiyo ikimenyana na watani, Yanga SC Oktoba 12.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia. |
0 comments:
Post a Comment